Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amewataka wazazi na walezi wa Kata ya Mrijo na Kelema Wilaya ya Chemba kuwapeleka watoto wenye ulemavu Shule na kutowafungia ndani kwani atakaye fanya hivyo atachukuliwa hatua za kisheria .

Akizungumza na Wananchi wa Kata hizo wakati wa muendelezo wa ziara zake katika Wilaya ya Chemba kwa lengo la kuangalia mahudhurio na uandikishaji wa wanafunzi tangu kuanza kwa muhula mpya wa masomo 2024 kukagua mradi wa ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum katika Shule ya Msingi Kelema Maziwani na ujenzi wa Shule Mpya ya Sekondari Mrijo Juu pamoja na kusikiliza kero na kuzitatua za wananchi wa Kata ya Mrijo Juu.

"Nitoe shime kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu toeni ile imani ya watoto walemavu kutokupata haki yao ya msingi,kama una mtoto mlemavu usimfungie ndani mpeleke Shule akasome serikali imesha mtengenezea mazingira.

"Kila mzazi atakaye mfungia mtoto nyumbani tutamchukulia sheria"
Ameelekeza Mhe.Senyamule

Sanjari na hilo, Mhe.Senyamule amesema Mkoa umejipanga kuhakikisha ufaulu unaongezeka pia kuongeza wasomi ndani ya Jiji , hivyo amewahimiza wananchi kuwajibika katika kuwapeleka watoto Shuleni na malezi kupitia kauli mbiu inayosema "Uwajibikaji wangu, ndio Msingi imara wa kuinua ubora wa Elimu na ufaulu Dodoma ".

Kwa Upande Wake,Kaimu Afisa Elimu Mkoa Mwl.Jane Mangowi amesema hali ya mahudhurio ya wanafuzi Shuleni na uandikishaji wa wanafunzi awali katika muhula mpya wa masomo kwa Kata hizo unaridhisha ambao umefika asilimia 75 hivyo amewahimiza wazazi na walezi kuwapeleka Shule.

Naye, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kelema Maziwani Mwl.Wiston Kuta akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa bweni la watoto wenye mahitaji maalum ameishukuru serikali ya awamu ya sita ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa mradi huo kwani utawanufaisha wanafunzi wenye mahitaji maalum kupata haki yao ya msingi ya kusoma.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...