Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa, amemuagiza Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Mohamed Besta kufanya tathmini ya eneo la Mtanana katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma ambalo leo Januari 9, 2024 lilijaa maji na kusababisha barabara hiyo kufungwa majira ya asubuhi.

Pia ameagiza kuwasilishwa kwa mkakati wa kudumu wa kudhibiti eneo hilo na maeneo yote korofi nchini ambayo hupata changamoto pindi mvua zinaponyesha.

“Mawasiliano ya barabara yamekuwa yakifungwa kutokana na maji kuvuka eneo la Mtanana, hivyo lazima tutafute suluhu ya kudumu ili barabara ipitike vipindi vyote vya mwaka”, amesisitiza Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amewaelekeza Mameneja wa TANROADS mikoa yote nchini kuhakikisha wanaendelea kukagua maeneo yote ya barabara na madaraja na kuchukua hatua za haraka kutokana na hitilafu zozote zinazoweza kusababisha kufunga kwa mawasiliano ya barabara.

Hata Hivyo, Bashungwa amewapongeza Mameneja hao kwa kazi nzuri wanazoendelea kufanya na kuchukua hatua za haraka pindi changamoto inapotokea.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...