NA MWANDISHI WETU, MICHUZI TV

SHIRIKA la Utangazaji limepata kibali na haki za kurusha matangazo ya fainali za michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) kupitia vyombo vyake vya habari ikiwemo Redio na Televisheni ambapo wataonesha mechi takribani 52.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 9,2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba amesema kuwa ni jukumu la msingi na ni dhima ya TBC kama chombo cha umma kuhakikisha Watanzania wanafikiwa na furaha itokanayo na burudani hususani za kimichezo.

“Sisi kama chombo cha taifa tuna dhima, tuna jukumu, yaani sisi tuna jukumu la msingi la kuhakikisha tunawaletea Watanzania furaha hasa kwenye michezo na ndio maana kwa mujibu wa taratibu za FIFA na hata CAF ni kwamba michezo hii mara nyingi inapelekwa kwenye chombo cha habari cha umma,” . Amesema .

Aidha amesema kuwa TBC, imekuwa na watangazaji mahiri wenye vipaji vya uhakika visivyokuwa na ubabaishaji hivyo kuwafanya watanzania kupata burudani ya michezo kwenye michuano hiyo kwa uhakika.

“Kuanzia enzi hizo ikiwa RTD hadi miaka ya sasa tuna watangazaji mahiri sana, tunaibua vipaji kila mwaka. Mwaka jana tulikuwa na Upete [Nazareth Upete], mnamfahamu, Upete yupo TBC. Tuna watu mahiri kwelikweli, kuna wakati watu wanadhani ubunifu ni ule ubabaishaji, mbwembwe za kibabaishaji, hapana, TBC tuna vijana mahiri kama Muhando ambao ni wabunifu na wanafanya vizuri,” Amesema Dkt. Rioba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...