Mapema leo Mbunge w Jimbo la Morogoro Mjini Mhe.Dokta Abdulaziz Abood amefanya ziara ya kushutukiza kwenye Kata ya mazimbu  lengo ikiwa ni kujionea miundombinu ya barabara namna ilivyo kwa kipindi hiki cha mvua. 

Akiwa maeneo ya balakuda kwenye Kata ya Mazimbu amejionea ubovu wa barabara hiyo inayoelekea chuo Kikuu Cha SUA Kampasi ya Mazimbu namna ilivyoaribiwa na mvua zinazoendele Sababu za kuaribika kwa barabara hiyo ni maji yanayopita mto ngerengere kuacha mkondo wake na kukatisha kwenye barabara hiyo. Jambo ambalo linasababisha watumiaji wa barabara hiyo kuvuka kwa shida na  jambo la hatari kwa afya za wananchi.

Mhe Mbunge ameahidi kuongea na TARURA ili kufanya haraka kurekebisha barabara hiyo na kuzuia maji kukatisha sambamba na uchimbaji wa mitaro.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...