MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imepanga  Februari 19,2024 kuanza kusikiliza kesi ya kujeruhi na kutoa lugha ya matusi inayowakabili wanandoa Bharat Nathwan (57), Sangita Bharat (54), ambao wanatuhumiwa kwa mashtaka manne. 


Kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa Februari 16,2023 mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Aaron Lyamuya, lakini imeshindikana kwa sababu hakimu huyo amepangiwa majukumu mengine ya kazi.


Wakili wa Serikali, Frank Michael amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga wa mahakama hiyo kuwa kesi hiyo imeitwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa na pia wanamashahidi wawili na wapo tayari kuendelea. 

"Mheshimiwa kwa leo tuna mashahidi wawili na tupo tayari kuendelea, lakini tulikuwa tunaomba tarehe nyingine ya usikilizwaji kwa sababu hakimu anayesikiliza kesi hii hayupo amepangiwa majukumu mengine," alidai Wakili Michael. 

Hakimu Kiswaga amewaonya mashahidi hao na kuwataka kufika mahakamani hapo Februari 19,2024 kwa ajili ya kutoa ushahidi wao.

" Mashahidi nawaonya kufika tarehe hiyo na huyo shahidi ambae amesema  tarehe hiyo hatakuwepo atawasiliana na wakili wa serikali atatoa ushahidi wake kwa njia ya mtandao 'Video Conference' kwa sababu vifaa vipo," amedai 

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa hao raia wa India wanaoishi Mrina - Kisutu, Dar es Salaam wanaotuhumiwa kwa mashtaka manne waliyoyatenda Julai 21,2023.

Katika shtaka la kwanza inadaiwa mshtakiwa Nathwan peke yake anadaiwa Julai 21, mwaka jana akiwa eneo la Mrina-Kisutu ndani ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam kinyume cha sheria alimsababishia madhara makubwa mke wa jirani yake, Kiran Lalit kwa kuzamisha kichwa chake kwenye ndoo ya saruji na kumjeruhi katika macho na sikio kwa kumpiga shingoni na kumsababishia maumivu.


Katika shitaka la pili la shambulio la mwili linalomkabili Nathwani (Chiku) peke yake, tarehe hiyo na eneo hilo alimsababishia madhara kwa kumshambulia jirani yake Lalit Ratilal katika mwili wake kwa kumpiga ngumi na mateke kichwani.

Katika shtaka la tatu na la nne mshtakiwa Sangita peke yake, anatuhumiwa kutoa matusi makubwa dhidi ya majirani zake, Lalit na Kiran  kitendo ambacho kilipelekea fujo kwa namna ambayo ingeweza kuleta uvunjifu wa amani.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...