NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya warsha Maalumu kwa Kushirikiana na kituo Cha Sayansi na Mazingira kutoka India (CSE India) yenye lengo la kutambua namna ya  mfumo wa ukaguzi wa mazingira unavyofanya kazi pamoja na kupeana uzoefu katika Usimamizi na Uhifadhi wa mazingira.

Akizungumza na waandishi wahabari leo Januari 25,2024, Afisa Mazingira Mwandamizi kutoka NEMC Bw. Novatus Mushi amesema kuwa mchakato wa usimamizi na Uhifadhi wa mazingira unahitaji uelewa mpana zaidi na taaluma mbalimbali ili kufanya ubobevu mkubwa katika ukaguzi huo.

"Ukaguzi wa mazingira lazima uhusishe wataalamu mbalimbali ili uweze kuzipata taarifa zote kwa ujumla wake ambazo utazihitaji kukuongoza katika ukaguzi wa mazingira ". Amesema Bw.Novatus.

Amesema kuwa NEMC wataendelea kujifunza kwa wageni wa mataifa mengine kwa kubeba mazuri ambayo wanayo na kuboresha katika huduma zao wanazotoa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Program ya Kupambana na Uchafuzi kutoka Viwandani Bw.Nivit Kumar wa Kituo Cha Sayansi na Mazingira India (CSE india) amesema kuwa anafikiri ni wakati sahihi kwa Mamlaka za Udhibiti wa Mazingira katika nchi za kiafrika kutumia ubunifu kuhifadhi mazingira ya nchi zao.

Aidha ameeleza kuwa walipofanya utafiti waligundua ripoti  za ukaguzi zilikuwa zikifanyika hazikuwa vizuri, hivyo wamejitahidi kuweka maelekezo vizuri jinsi ya kuchukua taarifa hizo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya (ECI) kutoka Kenya Bw. Gerphas Opondo amesema kuwa changamoto ya uchafuzi zilizopo Kenya na Tanzania ni zilezile, ijapokuwa Sheria za Uhifadhi zipo lakini watu bado wanakiuka taratibu hizo.

Warsha hiyo itafanyika kwa siku tatu na imejumuisha wadau mbalimbali kutoka mamlaka zinazosimamia mazingira kwenye mataifa mengine ya Afrika.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...