Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) kinawakaribisha wananchi wote katika Maonesho ya Biashara ikiwa ni Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba.

Akizungumza na Michuzi Blog Afisa Uhusiano Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Tulizo Chusi amesema anawakaribisha wanafunzi na wadau mbalimbali wa elimu ili kupata fursa mbalimbali pale watakapotembelea Banda la Chuo hicho ili kujua kozi zinazotolewa na chuo hicho.

Chusi amesema kuwa Sekta ya usafirishaji ina umuhimu mkubwa hasa katika kuendeleza na kuimarisha Sera ya uchumi wa Viwanda ambapo katika kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar wamekuja kutoa elimu hasa fani zinazotolewa  ambazo zinaweza kuinua uchumi wa Taifa hasa  kufanyakazi kwenye viwanda mbalimbali na kuongeza tija katika uzalishaji katika Sekta ya Usafirishaji.

“Wanafunzi wote tunawakaribisha sana waweze kufika hapa kwenye Banda letu kwa ajili ya kupata elimu na pia wanaweza wanaweza kupata huduma mbalimbali kupitia Website yetu ambayo ni www.nit.ac.tz ."  Amesema Tulizo.
Mkufunzi Mwandamizi kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Phabian Mongo (kushoto) akitoa maelezo Mkuu wa Kitengo cha huduma za Viwanja Vya Ndege kutoka Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) Thamalat Abeid (kulia) kuhusu kozi zinazotolewa na chuo hicho katika Banda la chuo hicho kwenye Maonesho ya Biashara ikiwa ni Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba.
Afisa Mitihani na Udahili Mwandamizi kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)   Lambert Rwegoshora  (kulia) akitoa maelezo kwa mwananchi aliyefika katika Banda la chuo hicho kwenye Maonesho ya Biashara ikiwa ni Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba.
Maonesho yakiendelea 
Watumishi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)  wakiongozwa na Afisa Uhusiano Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Tulizo Chusi wakiwa kwenye picha ya pamoja katika Banda la chuo hicho kwenye Maonesho ya Biashara ikiwa ni Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar yanayofanyika katika viwanja vya Fumba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...