NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

BANDARI ya Dar es Salaam katika kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba 2023 imefanikiwa kufanya huduma zaidi ya malengo yake ambapo imehudumia takribani meli 979 kati ya meli 792 zilizokuwa zimekusudiwa.

Ameyasema hayo leo Januari 9,2024 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mbossa wakati akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali katika ofisi za TPA.

Amesema kuwa katika kipindi hicho bandari imehudumia abiria takribani milioni 1 kati ya 900,000, makasha 990,000 kati ya lengo la kuhudumia makasha 500,000, huku mizigo ikiwa ni tani milioni 17.2 kati ya tani milioni 15.6 zilizokusudiwa.

Aidha Bw. Mbossa amesema kuwa kutokana na maboresho ya bandari meli hadi 12 zinahudumiwa kwa wakati mmoja, hivyo kupelekea wastani wa meli 100 kuhudumiwa kwa mwezi mmoja, kutoka meli 70 ndani ya mwezi mmoja.

Ameeleza kuwa, kutokana na mikakati mbalimbali ya serikali ya kukuza uchumi wa nchi kumepelekea kuwepo kwa ujenzi wa miradi mbalimbali na hivyo kuongezeka kwa kiwango kikubwa cha mizigo inayopita katika bandari hiyo.

Pamoja na hayo amesema kuwa ufanisi mkubwa unaofanywa kwenye bandari hiyo unachangia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi wa nchi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mbossa akijibu maswali ya waandishi wa habari katika Mkutano wa waandishi wa habari  leo Januari 9,2024 katika Ofisi za TPA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mbossa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Januari 9,2024 katika Ofisi za TPA Jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mbossa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Januari 9,2024 katika Ofisi za TPA Jijini Dar es Salaam.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Juma Kijavara akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Januari 9,2024 katika Ofisi za TPA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Mrisho Mrisho akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Januari 9,2024 katika Ofisi za TPA Jijini Dar es Salaam.


Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia Mkutano ulioandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) uliofanyika leo Januari 9,2024 katika Ofisi za TPA Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...