MAMLAKA ya Taifa ya Palestina imekiri kupokea Kwa Furaha Tamko la Kisheria la Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki

Mamlaka ya Palestina imepokea kwa furaha tamko lenye nguvu la kisheria lililotolewa na nchi ya Afrika Kusini katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki, likilaani uvunjaji mkubwa wa Mkataba wa Mauaji ya Kimbari unaofanywa na Israel.

Afrika Kusini ilisimama kwa nguvu na ilitoa ushahidi imara kuhusu jinsi Israel inavyokiuka makusudi majukumu yake chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari. Israel inatuhumiwa kufanya mauaji ya kimbari Gaza, kushindwa kuzuia mauaji hayo, na kuendeleza sera za mauaji ya kimbari. Huku Matamshi ya chuki na kichochezi yanayotumika, yakifanya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina kuwa na uhalali. Taarifa kutoka katika mamlaka ya serikali ya Palestine inasema Mauaji haya na jinai vinahitaji kusitishwa mara moja; watu wa Palestina wanahitaji kulindwa, na maisha ya binadamu lazima yaheshimiwe.

Huu ni wakati muhimu sana kwa Palestina na kwa dunia. Hatua hii ya Afrika Kusini inaonesha ujasiri na msimamo wa kanuni, ikitambua wajibu wake chini ya Mkataba wa Mauaji ya Kimbari. Ni wakati wa kukabiliana na mgogoro wa kihistoria, siyo tu kwa Palestina bali kwa ubinadamu wote na utawala wa sheria.

Mfumo wa kimataifa umeshindwa kutimiza majukumu yake ya kudumisha amani na usalama wa kimataifa. Hali hii imeibua mgogoro mkubwa ukitishia uaminifu na uhai wa mfumo huo. Ukiukwaji unaofanywa na Israel dhidi ya watu wa Palestina ni jinai ambayo inashangaza dhamiri ya dunia, na inahitaji hatua za haraka kwa ajili ya haki.


Tamko linaeleza kuwa Afrika Kusini imechukua hatua hii kwa dhamira ya kuheshimu sheria, badala ya kuwa mtazamaji mnyonge wa kuvuruga kanuni za kimataifa kwa maslahi ya kisiasa. Mamilioni ya watu wanaoandamana mitaani kote duniani wanakubaliana na hatua hii ya kisheria. Watu wa Palestina wanapata matumaini katika uthibitisho kwamba uadilifu na ujasiri wa kimaadili vinaweza kuushinda ubaguzi na uchochezi wa vita.


Hii ni kesi ya kisheria, sio kisiasa. Sheria itakuwa kipimo cha haki, siyo ubaguzi wa chuki au upendeleo. Jaribio lolote la kuharibu mchakato huu wa kihistoria kwa kisiasa na matumizi ya maneno yenye upendeleo litapingwa na kuwekwa wazi. Taarifa inasema.


Mamlaka ya Palestina ina imani kwamba Mahakama ya Kimataifa ya Haki itasimama imara, italinda uhuru wake, na kukutana na majukumu yake kwa heshima kwa sheria, ikikabiliana na ukwepaji wa sheria.


Hatwezi kukaa kimya mbele ya uhalifu wa kivita, jinai dhidi ya ubinadamu, na mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina. Tunaitaka dunia kusimama pamoja kwa ajili ya uwajibikaji na haki, kulinda watu wa Palestina na kuhakikisha heshima na haki zao zinapatikana. Taarifa inasema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...