Waziri wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango wakati akizinduzia hati fungani ya kijani ya miundombinu ya maji Mkoani Tanga ambao utasaidia kwenye Sekta ya Afya ikiwa ni pamoja na huduma za Afya ya Uzazi mama na mtoto.

Uzinduzi huo umefanyika leo Februari 22, 2024 kwa jitihada za Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini Mhe. Ummy Mwalimu ambapo mradi huo utaongeza upatikanaji wa maji kwa wastani wa lita Milioni 15 inakua jumla ya upatikanaji wa maji lita Milioni 60 katika Jiji la Tanga Mjini, Wilaya jirani za Muheza na Mkinga baada ya lita 45 za awali.

Mradi huo umeanza baada ya uzinduzi wa hati fungani ya Kijani ya Miundombinu ya Maji Tanga Katika eneo la Mabayani Jijini Tanga siku ya jana ukiwa na lengo la uboreshaji wa upatikanaji wa maji wenye gharama zaidi ya Bilioni 53 ambao utazalisha lita milioni 60 kwa Mkoa wa Tanga.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...