Raisa Said,bumbuli

Mbunge wa Jimbo la bumbuli January Makamba ametoa msaada Wa majiko ya gesi 123 katika shule za Sekondari 24 na Msingi 99 zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Mkoani Tanga.

Msaada huo umetolewa wakati Wa kikao Cha tathimi ya elimu na wakati wakupongeza shule zilizofanya vizuri Mwaka 2023 nazilizotoa wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya darasa la Saba mwaka Jana.

Makamba ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje ametoa mitungi hiyo ya gesi kuunga mkono juhudi za Rais Samia ambaye ameweka malengo kuwa ifikapo mwaka 2030 asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia gesi safi ya kupikia.

Wakipokea majiko hayo ya gesi walimu hao yaliyokabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Lushoto Amir Shehiza na Mkurugenzi Mtendaji Wa Halmashauri Baraka Zikatimu walisema wanashukuru kwa kupata msaada huo ambao umekuja wakati muafaka kwao.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...