

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa pole Mjane wa Marehemu Mama Regina Lowassa mara baada ya kuwasili katika eneo la mazishi, nyumbani kwa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa, Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine katika mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.
.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa, Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.


Mjane wa Marehemu Mama Regina Lowassa akisali mbele ya jeneza lenye mwili wa Waziri Mkuu Mstaafu Hayati Edward Ngoyai Lowassa nyumbani kwake Monduli Mkoani Arusha tarehe 17 Februari, 2024.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...