Na Mwandishi wetu - Ruvuma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho amesema Serikali imefanya Maboresho makubwa katika sekta ya elimu katika kipindi cha miaka mitatu.

Kauli hiyo ameitoa Wakati alipoongozana na Wenyeviti wa Mashina wa CCM katika kata ya Parangu, Mpandangido, Kilagano na Maposeni kujionea utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwenye ujenzi wa Miundo Mbinu ya Mambweni na Madarasa uliyofanyika katika shule ya sekondari Maposeni na Mtopesi katika Halmashauri ya Songea Mkoani Ruvuma.

Waziri Mhagama amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongoza Rais Samia imetoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya elimu, ili kupunguzia wananchi adhaa ya kuchangishana michango kwa ajili ya ujenzi.

Katika shule ya Sekondari Maposeni kuna ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya 40, ambapo kuna madarasa ambayo ujenzi umekamilika na mengine yako mbioni kujengwa.

"Hivyo basi jamii inawajibu wa kumlinda mtoto wa kike na kumlinda mtoto wa kiume kwa kuwapatia elimu bora itakayosaidia kujenga Jamii yenye weledi," alisema.

Ameongeza kusema zawadi nyingine aliyotupatia Rais ni kuhakikisha anafuta ada na kusaidia watoto wengi kwenda shule.

"Kutokana na ongezeko la wanafunzi, tunahitaji kuongeza miundo mbinu ya elimu kwa ajili ya vijana wetu, Serikali inaandaa mitaala mpya ambayo itasaidia kuwapa elimu ya ufundi vijana wetu waweze kupata ujuzi " alibainisha

Sambamba na hilo Halmashauri ya Songea Vijijini, serikali itajenga chuo kikubwa cha Ufundi cha VETA katika Kata ya Liganga ili kuwezesha vijan kupata elimu ya ujuzi katika chuo hicho.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Songea Vijijini Menace Komba amesema tayari wameshaanza utaratibu wa kuomba wizara ya elimu ili kupata kibali cha kubomoa majengo ya zamani ya shule ya sekondari Maposeni na Mpitimbi ili kujenga Madarasa mapya.

"Uamuzi huo umeafikiwa na Halmashauri ya Songea Vijijini ili kuipatia shule ya sekondari Maposeni pamoja na Mpitimbi muonekano mzuri na wakuvutia,"alisema.

Awali Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mwalimu Dismass Nchimbi akizungumza mbele ya ujumbe wa wenyeviti wa Mashina alisema serikali imefanya mambo mengi katika shule ya sekondari Maposeni.

"Tumepata mradi wa ujenzi wa Mambweni 2, na Madarasa 4 na vyoo matundu 10 mradi unaofadhiliwa na Barick katika Jimbo la Peramiho, " alisema.

Serikali kwa kupitia Mbunge wa Peramiho amesaidia pia ujenzi wa jengo jipya la utawala ambalo limegharimu kiasi cha shilingi million 74 na ujenzi wake umefikia kwenye lenta.

Akitoa neno la shukrani Mwanafunzi, Ahad Antony Bugari umeshukuru serikali kwa kuimarisha Miundo Mbinu ya elimu katika shule ya sekondari Maposeni.

Amemshukuru walimu wa Maposeni kwa kusimamia vizuri ujenzi wa Miundo Mbinu ya elimu katika sekondari ya Maposeni.

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho  akizungumza na Mabalozi wa kata ya Mpandangido, Peramiho, Parangu, Maposeni na Kilagano katika Halmashauri ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho, akiongozana na Wenyeviti wa Mashina wakikagua Mradi wa ujenzi wa Bweni katika shule ya sekondari Maposeni katika Halmashauri ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma.
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) Peramiho akiwa katika Picha ya Pamoja na wenyeviti wa Mashina Katika shule ya sekondari Mtopesi Halmashauri ya Songea  Vijini Mkoani Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...