Na Karama Kenyunko Michuzi Tv.

BUNGE la jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kukusanya fedha za kujenga shule ya wavulana ya vipaji Maalum kupitia mashindano ya mbio 'marathon'

Naibu Spika wa Bunge Mussa Zungu amesema hayo leo Machi 18, 2024 katika Ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Naibu Spika Zungu amesema kuwa huo ni muendelezo kwa bunge kujenga shule ambapo tayari muhimili huo umejenga shule ya sekondari ya wasichana jijini Dodoma iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni 2

Mbali na kujenga shule hiyo bunge liliwachangia madawati yenye thamani ya shilingi 6 Bilioni kwa ajili ya shule mbalimbali nchini.

Amesema kuwa Bunge litachangisha vifaa na fedha kupitia marathon hiyo itakayofanyika tarehe 13 Aprili 2024 jijini Dodoma.

Amesema kuwa washiriki wa mbio hizo watajisajili kwenye Tovuti ya Marathon.bunge.go.tz na atalipia kiasi cha Shilingi 40,000. Kupitia mitandao mbalimbali ya simu pamoja benki ya NMB na CRDB.

"Mbio za Bunge Marathon zinatarajiwa kushirikisha wakimbiaji 5000 kutoka ndani na nje ya nchi. Zitakuwa na umbali wa nusu Marathon (kilomita 21) kilomita 10 na kilomita 5 zitakazobeba kauli mbiu ya 'Shiriki Michezo kwa Maendeleo ya Taifa letu" amesema Zungu.

Amesema kuwa mshindi wa kwanza mbio za Kilometa 21 atazawadiwa kiasi cha shilingi Milioni tano, wa pili ataondoka na shilingi Milioni tatu na mshindi wa tatu atajinyakulia kiasi cha shilingi Milioni moja na nusu huku watakaoshika nafasi ya 4 hadi 10 watapewa kifuta jasho kiasi cha shilingi laki mbili.

Mbio za kilometa 10 , mshindi wa kwanza atazawadiwa kiasi cha shilingi Milioni mbili, wa pili shilingi Milioni, moja na nusu na mshindi watatu atajipatia kiasi cha shilingi Milioni moja huku washindi wa 2 hadi wa 10 watavuna kiasi cha shillingi laki moja.

Mbio za kilomita 5 mshindi wa kwanza atazawadia kiasi cha shilingi Milioni moja na nusu, wa pili atapata shilingi milioni moja, watatu shilingi laki tano huku watakaoshika nafasi ya 4 hadi ya 10 watapewa kiasi cha shilingi 50,000.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...