Na Janeth Raphael - MichuziTv -Dodoma.

Naibu Waziri wa ujenzi Godfrey Kasekenya (MB) amewakumbusha wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuzingatia maadili katika utendaji wa kazi zao.


Kasekenya amezungumza hayo leo wakati akifungua kikao cha Baraza la wafanyakazi TEMESA katika ukumbi wa ofisi hizo makao makuu Dodoma.

"Mtumishi wa TEMESA anayefanya biashara na TEMESA kwa kificho au waziwazi Kupita kampuni yake au ndugu zake na kupelekea mgongano wa maslahi hana tofauti na abiria anayetoboa mtumbwi katikati ya safari" - Kasekenya


Kasekenya amesema kuwa watumishi wa aina hiyo hawataiwezesha TEMESA mpya hivyo kupitia kwao wafanyakazi anawasihi wote kutokujiingiza wala kujihusisha na vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa Umma na atakayebainika atachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa sheria zilizopo.

Kasekenya amesema TEMESA ipo katika hatua mbalimbali za kuboresha utendaji kazi ikiwa ni pamoja na kuandaa mkakati wa kuboresha utendaji kazi kwa miaka 10.

"Pamoja na kazi nzuri zinazoendelea kufanyika niendelee kusisitiza suala la uwajibikaji na na natoa rai kwa TEMESA kwani tumepewa dhamana kubwa na Serikali "- Kasekenya

Aidha Naibu waziri huyo wa ujenzi amewakumbusha watumishi wa TEMESA kuwa wao kama wakala wanatakiwa kujiendesha kibiashara hivyo wanapaswa kuwa na mtazamo huo na kuwaelewesha watumishi wanaowawakilisha waache kufanya kazi kwa mazoea na kuzingatia kuwa biashara ni ushindani
"Kuweni wabunifu katika mifumo ya TEHAMA na mbinu mbalimbali za biashara"

Hata hivyo Kasekenya amelikumbusha baraza hilo kuwa Serikali ya awamu ya sita kupitia ilani ya Chama Tawala (CCM) imeweka malengo mbalimbali, na utekelezaji wa ilani hiyo unawategemea watumishi wa Umma.

Awali Mwenyekiti wa Baraza hilo la wafanyakazi ambaye pia ni mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro Kilahala amesema Baraza la wafanyakazi ni chombo au daraja muhimu la ushauri na majadiliano sehemu ya kazi linalosaidia pande zote mbili za mwajiri na mwajiriwa kuboresha mazingira ya kazi ya taasisi na kuleta ufanisi na tija.

"Kupitia Baraza la wafanyakazi wajumbe wanapata nafasi ya kuushauri wakala juu ya mambo muhimu yanayohusu maslahi ya wafanyakazi." - Kilahala
 

Naibu waziri wa Ujenzi Godfrey Kasekenya akizungumza wakati alipofungua kikao cha Baraza la wafanyakazi la Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Leo jijini Dodoma.
 

Mtendaji Mkuu wa Walaka wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro Kilahala akizungumza katka Baraza la wafanyakazi TEMESA leo jijini Dodoma

 

Sehemu ya wajumbe wa Baraza la wafanyakazi TEMESA
 

Naibu Waziri wa ujenzi Godfrey Kasekenya akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Baraza la wafanyakazi TEMESA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...