Raisa Said,Tanga

WAKALA wa Mabasi Yaendayo Kasi (DART) umetoa ufafanuzi kwa watanzania kuwa mchakato wa kuingia mazungumzo na kampuni binafsi ya Emirates National Group (ENG) ya Abu Dhabi kuendesha shughuli za mabasi yaendayo kasi jijini Dar es Salaam haukuanza katika kipindi hiki cha awamu ya sita, bali ulianza mwaka 2017 wakati wa serikali ya awamu ya 5.

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa DART, Dk Athumani Kihamia alipokuwa akifafamua kuhusu mchakato huo kufuatia baadhi ya watu kuanza kujadili uwepo wa mchakati huo ambao unahusu kampuni ya ENG kushinda zabuni hiyo, katika mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa makao makuu ya Klabu ya Waandishi wa Habari jijini Tanga.

Alieleza kuwa huduma ya usafiri wa mabasi yaendayo kasi hivi sasa inatolewa na mtoa huduma wa mpito ambaye ni kampuni ya UDART ambayo hivi sasa ina mabasi 110.

Dk Kihamia alisema kuwa kumekuwa na dhana potofu ambayo inasambazwa na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi kuwa mchakato huo umeanza katika kpindi hiki cha awamu ya sita, inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan kitu ambacho si kweli.

Alieleza kuwa mchakato wa mazunguzo ya kutafuta mbia wa kuendesha shughuli za usafirishaji kupitia mfumo wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es salaam ulianza mwaka 2017 wakati serikali ilipotangaza tenda za kutoa huduma hiyo kwa watoa huduma binafsi chini ya sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi (PubliC Private Partnership-PPP).

Majadiliano yalianza lakini walishindwana kutokana na kutokubaliana katika baadhi ya vipengele ikiwemo kipenegele cha bei (nauli) na suala la uchaguzi wa msuluhishi kuwa wa kitaifa au wa kimataifa.

“Muda ulipita lakini mwaka 2020 tenda ikatangazwa tena ambapo kampuni 40 zilileta maombii yao ikiwemo ENG na bado kampuni hiyo ikaongoza katika vigezo na machakato ukaendelea hadi kufikia hatua ya kukaribia kusaini mkataba wa miaka 12,” alisema.

Dk Kihamia alisema kuwa, hata hivyo, kipengele cha msuluhishi kikaendelea kuleta tabu, suala la bei na DART kuweka kipengele cha kuvunja mkataba wakati wowote kama isiporidhiswa na utendaji.

Baada ya serikali kufanya mabadiliko katika sheria ya PPP suala la msuluhishi limepata muafaka na msuluhishi wa kimataifa ameruhisiwa. Vivyo hivyo suala kuvunja mkataba wakati wowotte limeondolewa.

Alisema kuwa hivi sasa mazungumzo yamebaki masuala ya kiufundi na yapo katika hatua za mwisho. Alisema yakikamailika ENG italeta mabasi 177 kwa ajili ya kutoa huduma kaktika mradi wa awamu ya kwanza njia ya kimara hadi mjini

Aisema kuwa mkataba unatazamiwa kusainiwa mwezi ujao, April na ifikapo mwezi Septemba na Oktoba mabasi hayo yanategemewa kuiingizwa nchini tayari kwa kuanza huduma kama alivyoelekeza kwa msisitizo na Mheshimiwa Mohammed Mchengerwa ambaye ni Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa.

Alisisitiza kuwa mtoa huduma wa hivi sasa (UDART) bado atandelea kutoa huduma yake kwa sababu bado kuna maeneo mengi sana ya jiji yanayohitaji huduma hivyo ambayo inakwenda kwa awamu.

“Tuna nia yakupanua huduma zetu si kwa ajili ya jiji la Dar es salaam pekee, bali katika majiji yote nchini,” alisema Dk Kihamia.

Hata hivyo alisisitiza kuwa hii ni awamu ya I na awamu zipo zaidi ya 6 kwa Dar es Salaam na bado kuna maeneo mengine katika majiji ya Dodoma, Mwanza, Mbeya hivyo makampuni mengi zaidi kutoka kote duniani na ya hapa nchini yaombe tenda zikitangazwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...