NA VICTOR MASANGU KIBAHA

Katibu wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Issack Kalleiya ametimiza ahadi yake kwa vitendo kwa kutoa msaada wa magongo kwa kijana mmoja anayeishi katika kata ya Msangani.

Kijana huyo ambaye anajulikana kwa jina la John William amepatiwa msaada huo baada ya kupata ajali ya kupushiwa na Lori hivi karibuni na kupelekea mguu wake wa kulia kuvunjika kwa chini.

Katibu huyo wa CCM alike da kutoa msaada huo akiwa ameambatana na viongozi mbali mbali wa chama sambamba na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibaha mji Mwalimu Mwajuma Nyamka pamoja na baadhi ya wananchi wengine.

Katibu huyo alisema kwamba alipokea kwa masikitiko makubwa juu ya taarifa hiyo ya kijana wa CCM kupata ajali hivyo aliahidi kwenda kumuona pamoja na kumpatia msaada huo wa magongo.

"Kwa kweli mimi kama kiongozi niliguswa sana na tukio hili la kijana wetu wa ccm ambaye kwa kweli nikaona kuna umuhimu kumsaidi kwa hali na mali magongo ambayo yataweza kumsaidia katika kufanya mazoezi ya kutembea,"alifafanua Katibu huyo.

Kadhalika alisema kwamba kijana huyo amekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na vijana wenzake kwa lengo la kukilinda na kukiimarisha chama katika mambo mbali mbali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Kibaha mji Mwalimu Mwajuma Nyamka naye alifika nyumbani kwa kijana huyo kwa ajili ya kumona na kumfariji.

Naye Kijana huyo John William aliyepata ajali alimshukuru kwa dhati Katibu wa CCM kwa moyo wake wa upendo wa kumpatia magongo hayo na kuwashukuru viongozi wote wa CCM waliokwenda kumjulia hali na kumpa pole.Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...