Na Yeremias Ngerangera....Namtumbo.
Wakiongea
katika mkutano wa hadhara wa Kijiji hicho ,wananchi wa Kijiji Cha
Mdwema walisema wanaridhia Mpango wa matumizi Bora ya ardhi ya Kijiji
Chao.
Greyson Choma ni mwenyekiti wa Kijiji Cha
Mdwema Pamoja na kuwashukuru wananchi wa Kijiji chake kuridhia
kupitisha Mpango wa matumizi Bora ya ardhi ya Kijiji Chao , aliwashukuru
zaidi wafadhili CARITAS waliogharimia Mpango huo .
Choma
Pamoja na shukrani hizo aliwataka wananchi wa Kijiji hicho kufuata
sheria,kanuni,miongozo na taratibu zilizowekwa katika kusimamia Mpango
wa matumizi Bora ya ardhi .
Faustin Chuma
mwananchi wa Kijiji Cha Mdwema Pamoja na kuridhia kupitisha Mpango huo
aliiomba idara ya ardhi kupanda mawe kwenye mipaka kati ya Kijiji Chao
na vijiji vingine ili kulinda ardhi Yao iliyotengwa Kwa ajili ya msitu
ili wananchi wa vijiji vingine wasiingie katika maeneo hayo Kwa madai ya
kutojua maeneo Yao.
Afisa Mazingira wa
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Kelvin Mnali aliwaambia wananchi hao
kuwa sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 inakataza kufanya shughuli za
kibinadamu katika vyanzo vya maji na maeneo ya milima huku akiwataka
wananchi hao Kujua sheria hiyo katika kusimamia Mpango wa matumizi Bora
ya ardhi ya Kijiji Chao.
Mary Albert Mratibu wa
Mpango kutoka CARITAS ambao ndio waliofadhili Mpango huo alisema Kwa
hatua za awali maeneo ya mipaka ya Kijiji hicho yatawekewa vibao
kuonesha Shughuli inayotakiwa kufanywa katika eneo husika huku akiitaja
idara ya ardhi ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kuandaa ramani na
kupanda mawe kuonesha mpaka wa Kijiji hicho na vijiji vingine.
Zakaria
Kapinga Afisa ardhi mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo
aliwaambia wananchi wa Kijiji Cha Mdwema kuwa Mpango wa matumizi Bora ya
ardhi ya Kijiji chao utakuwa wa Miaka kumi kuanzia mwaka huu 2024 mpaka
mwaka 2034 na baada ya Miaka 10 Mpango huo unaweza ukafanyiwa mapitio.
CARITAS
ni Taasisi isiyo ya kiserikali ambayo inajishughulisha na vikundi vya
ufugaji wa Nguruwe na kilimo Cha mazao kupitia vikundi vidogo vidogo vya
wakulima wa Kijiji Cha Mdwema ambapo Taasisi hiyo inatumia kiasi Cha
shilingi milioni 12 kukifanya Kijiji hicho kuwa katika Mpango wa
matumizi Bora ya ardhi yake ya Kijiji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...