Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha.
WAKAZI
 wa Kitongoji cha Kisabi , Mlandizi,Kibaha Vijijini , Mkoani Pwani 
wanaotakiwa kupisha eneo hilo na kuhamia Kikongo eneo lenye ekari 1,000 
lililotolewa na Serikali wamegomea kuhama wakidai ugumu wa kuanza maisha
 mapya.
Hayo yalielezwa 
na wakazi hao akiwemo Esther Shishima, Nuhu Msheka ,Daudi Mwasumbi 
wakati Mkuu wa wilaya Kibaha Nikkison Simon alipomwakilisha Mkuu wa mkoa
 wa Pwani Alhaj Abubakar Kunenge kwenye mkutano wa kusikiliza na kutatua
 kero za wananchi.
Shishima aliiomba, Serikali kuwaacha waendelee kuishi katika eneo hilo kwani wamechoka kuhamahama na watoto kama wakimbizi.
"Tunaambiwa
 tuhame kuwa kuna zuio la kimazingira tuache kuendelea kujenga,eti 
sheria imekataa ,sasa mbona wapo wenzetu eneo la  Halmashauri wanajenga 
na wanamudu hiyo hali ,basi na sisi tutaweza,watuache tumechoka 
kuhangaika na watoto" alifafanua Shishima.
Nae
 Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kisabi ,Yahaya Matata alieleza awali 
waliovamia eneo hilo walikuwa 41 baadae wakaongezeka na kufikia 91 sasa 
wameongezeka wapo zaidi ya 300.
Mkuu
 wa wilaya ya Kibaha , Nikkison aliahidi kuyafikisha maombi hayo sehemu 
husika kwa lengo la kutoa maamuzi zaidi ingawa alisisi kuwa kutokana na 
ushauri wa kitaalam kimazingira eneo hilo si rafiki kwa makazi hiyo 
wananchi wanapaswa kuhama.
Nikkison
 alieleza Serikali ya mkoa ilitoa ekari 1,000 kwa wakazi wa Kisabi ili 
lipimwe viwanja na kugawiwa kwa wakazi wanaoishi kwenye eneo Oevu.
Nikkison
 alifafanua kuwa, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa mazingira- 
NEMC lilitahadharisha juu ya eneo hilo kutumika kujengwa makazi ya 
binadamu kwa kuwa ni oevu linaloweza kusababisha madhara yatokanayo na 
mafuriko kikiwa ni pamoja na uwezekano wa nyumba kutitia.
Kutokana
 na hali hiyo Ofisi iliamua kutafuta eneo rafiki linalofaa kwa makazi ya
 binadamu ambalo alieleza linapatikana katika kijiji cha Kikongo na sasa
 maandalizi ya upimaji unaendelea ili wakazi hao wapewe viwanja.






Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...