Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam. Tarehe 01 Machi 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akitoa salamu za pole kwa familia, viongozi na wananchi kwa ujumla wakati wa kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam. Tarehe 01 Machi 2024.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Mama Sitti Mwinyi wakati wa kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam. Tarehe 01 Machi 2024.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed Ali wakati alipowasili Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam kushiriki kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi. Tarehe 01 Machi 2024.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed Ali akitoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam. Tarehe 01 Machi 2024.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amewaongoza waombolezaji katika kutoa heshima za mwisho wakati wa kuaga mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam.

Akitoa salamu za pole kwa waombolezaji, Makamu wa Rais amesema Hayati Ali Hassan Mwinyi atakumbukwa kwa kuwa kisima cha hekima, chemichemi ya elimu na shule ya uzalendo uadilifu na uongozi. Amesema Hayati Mwinyi alijitoa kwa dhati kulitumikia Taifa kwa moyo wake wote na kutoa mchango mkubwa kwa nafasi zote alizoshika katika utumishi wa umma.

Makamu wa Rais ameongeza kwamba Hayati Ali Hassan Mwinyi alikuwa kielelezo cha kutetea na kudumisha umoja wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, alikuwa na karama kubwa ya uongozi na alizingatia kwa dhati masharti ya uongozi ikiwemo uwajibikaji pamoja na kutoa mchango mkubwa katika kukuza matumizi ya lugha ya kiswahili na kuifanya kutambulika na kutumika kimataifa.

Halikadhalika Makamu wa Rais amesema Hayati Ali Hassan Mwinyi aliasisi mageuzi ya kiuchumi na kisiasa hapa nchini, alijijengea sifa kubwa katika kuhamasisha kilimo bora pamoja na kuwa na bidii katika kumwabudu Mwenyezi Mungu.

Tukio la kuagwa kwa Mwili wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam limehudhuriwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Abiy Ahmed Ali, viongozi mbalimbali wa kitaifa, Mabalozi wa Mataifa mbalimbali, Viongozi wa Ulinzi na Usalama, Viongozi wa Dini mbalimbali pamoja na Wananchi.

Imetolewa na Ofisi ya Makamu Rais 01 Machi 2024 Dar es salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...