Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete  akizungumza kwenye hafla ya kumuaga Hayati Alhaji Ali Hassan Mwinyi iliyofanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam leo Machi Mosi, 2024.
Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitoa heshima zake za mwisho.
Mama Sitti Mwinyi (Mjane wa Marehemu) akitoa heshima  zake mbele ya jeneza la Hayati Mwinyi.
Bi Khadija Mwinyi  (Mjanewa marehemu) akitoa heshima zake mbele ya jeneza  la Hayati Mwinyi.

Na Khadija Kalili
RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa Hayati Alhaji Ali Hassan Mwinyi alikua Kiongozi asiyejikweza, alikua mtu mwenye mapenzi na watu wote.

Kikwete amesema hayo leo Machi mosi, 2024 alipozungumza na viongozi mbalimbali pamoja na waombolezaji waliohudhuria hafla ya kumuaga kitaifa Hayati Alhaji Ali Hassan Mwinyi kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

"Mwinyi aliishi maisha ya kawaida ya uungwana, alikua msikivu na alikua ni mtu wa kupokea maoni na zaidi ya yote alinifundisha kuwa na maamuzi hasa kwenye vitu vyenye maslahi ya taifa yeye ndiye baba wa mageuzi ya uchumi na kisiasa hapa nchini." Amesema Rais Mstaafu Kikwete.

Naye Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa awamu ya pili Mstaafu Joseph Warioba akimzungumzia Hayati Mwinyi amesema kuwa "Leo ni siku ya majonzi ya kuondokewa na mzee Mwinyi lakini pia ni siku ya furaha ya kusherehekea maisha yake kwa mengi aliyoyafanya wakati alipolitumikia taifa hili, kwani amekuwa na juhudi nyingi za kuleta maendeleo hasa kwenye nyanja ya kiuchumi na kisiasa."Amesema Warioba.

Wakati huohuo Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amemuelezea Hayati Mwinyi kwa kusema kuwa "Sote ni mashahidi kwamba Hayati Ali Mwinyi alifanya jitihada za kuitoa nchi ya Tanzania kwenye mfumo wa chama kimoja kwenda kwenye mfumo wa vyama vingi" amesema Kinana.

Ameongeza kwa kusema kuwa suala hili halikuwa rahisi vilevile alitupeleka kwenye uchumi huria alifanya yote haya mengine mengi huku akimshirikisha Hayati baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa lengo la kuhakikisha kwamba mabadiliko yanafanyika kwa utulivu na kulinda amani na utulivu wa nchi.

Kabla ya kupelekwa Uwanja wa Uhuru mwili wa Alhaji Mwinyi umeswaliwa katika msikiti wa BAKWATA na maziko yatafanyika kesho Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...