*Mchechu aweka mipango mikakati na Taasisi ambazo serikali ina hisa chache
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Serikali imesema imeamua kujenga sekta binafsi nchini ili isaidie katika kuchochea maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja kuongeza thamani ya bidhaa mbalimbali.
Hayo ameyasema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo wakati wa hafla ya kufunga Mkutano wa Msajili wa Hazina uliohusisha Wakurugenzi na wajumbe wa Bodi za Taasisi ambazo Serikali ina hisa chache, hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere , Kibaha mkoani Pwani
Amesema kuwa serikali imefanya uwekezaji katika Taasisi ambazo zinatakiwa kubadili mtazamo wa kwenda kibiashara.
Profesa Kitila amesema kuwa Taasisi ambazo serikali ina hisa chache zinawajibu wa kushauri serikali sehemu ambazo taasisi hazifanyi vizuri..
Amesema kuwa Wakurugenzi na wajumbe wa Bodi wa Taasisi ambazo ina hisa chache kuendana na serikali na kushauri huko katika kwenda na mipango ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan juu kuongeza thamani ya bidhaa ili ziweze kuwa na soko kwenye masoko mbalimbali nje ya nchi.
Mkumbo alibainisha kwamba ana imani mpango huo wa dira ya Taifa utaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kwa kushirikiana na sekta binafsi.
"Kitu kikubwa kama serikali kwa tunajipanga kwa ajilli ya kuandaa dira mpya ya Taifa kwa kushirikiana na wataalamu mbali mbali ili kuweza kuwa na mpango wenye kuleta tija siku zijazo "alisema Professa Mkumbo
Kwa upande wake Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu alisema kwamba mkutano huo umeweza kuwakutanisha mashirika ya umma na kufungua fursa za kupanga mipango ambayo itasaidia nchi kupata maendeleo kwa kuongozwa na maazimio.
Mchechu alibainisha kwamba katika wameweza kujadili kwa pamoja namna ya kushirikiana na serikali katika kukuza ya uchumi na maendeleo kulingana mazingira yaliyopo
Mchechu amesema kukutana na taasisi ni pamoja kuongeza tija kwa kile ambacho kinajadiliwa
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Amon Nnko amesema wamepitisha maazimio matano katika mkutano huo ambayo yatasaidia kukuza uchumi wa nchi
Aliongeza kuwa katika maazimio hayo ni kuweza kupambana na mwenendo wa hali ya uchumi duniani kufanya mafunzo ya awali,pamoja na kulinda maslahi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, akizungumza wakati kufunga Mkutano wa Taasisi ambazo Serikali ina Hisa chache ulioratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina uliofanyika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha mkoani wa Pwani.
Msajili wa Hazina Nehemia Mchechu, akitoa maelezo kuhusiana na Mkutano wa Taasisi ambazo serikali ina hisa Chache juu umhimu wake katika kukuza uchumi ,Kibaha mkoani Pwani
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Kida, akitoa hotuba kuhusiana na mikakati ya Ofisi hiyo katika uchocheaji wa uchumi nchini.
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, Amon Nnko, akizungumza wakati akitoa maazimio ya mkutano wa Taasisi ambazo Serikali ina Hisa Chache.
Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo na Wafanyakazi wa Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...