Katika kuanzimisha wiki ya Maji Duniani Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu limeiyasa Jamii kuwa mstari wa mbele kusimamia mapango wa kulinda na utunza vyanzo vya maji.

Wito huo umetolewa March 16,2024 na Meneja idara ya Mazingira Bondi ya maji Bonde la Wami Ruvu Mhandisi Paschal Qutaw, kwenye uzinduzi WA wiki ya Maji mjini Morogoro ulioambatana na uzoezi la usafi eneo la Mto Kikundi.

Msisitizo uliopo ni jamii kushiriki moja kwa moja katika kulinda na kutunza vyanzo vya maji, kupunguza athari zitokanazo na uharibifu wa vyanzo vya maji.

Sophia Mwenda ni Mkuu wa Maabara ya Ubora wa Maji Morogoro amesema athari za uharibifu wa vyanzo vya maji ni pamoja na kupanda Kwa ghalama za ankara za maji linalosababishwa na ongezeko la matumizi ya Sawa za kusafisha Maji katika mitambo.

"Nitoe wito Kwa jamii kutunza vyanzo vya maji kwani uharibifu wa vyanzo vya maji unasabisha kupungua Kwa ubora wa Maji hivyo mamlaka zinazosambaza Maji zinatumia ghalama kubwa katika kusafisha Maji na kufanya bili za Maji pia kupanda kutokana na kuongezeka Kwa ghalama za uendeshaji". Alisema Bi Sophia

Kwa ipande wao baadhi ya Wakazi wa Mkoa wa Morogoro wamesema wanatambua umuhimu wa mpango wa kulinda na kutunza vyanzo vya maji unaolenga kunusuru kupanda kwa Ankara za maji na upatikanaji wa maji safi na salama hivyo watashirikiana na mamlaka zinazohusika kilinda vyanzo

Wiki ya maji huadhimisha kila ifikapo machi 16 hadi 22 kila mwaka ambapo kwa mwaka huu wa 2024 kitaifa yanafanyika Jijini Dododma na kupabwa na kauli mbiu isemayo Uhakika wa maji kwa amani na utulivu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...