Na Mwandishi Wetu

MKURUGENZI  wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) Latifa Khamis ameongoza upokeaji na majadiliano ya matokeo utafiti wa awali wa hali ya biashara nchini.

Taarifa iliyotolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Uhusiano kwa Umma na Masoko Tantrade, Lucy Mbogoro imeeleza kuwa zoezi hilo limefanyika leo Machi 11, 2024 katika ukumbi wa Kilimanjaro sabasaba jijini Dar es Salaam.

Akizungumza  wakati wa upokeaji wa matokeo ya utafiti huo, Latifa amesema utafiti huo wa hali ya biashara nchini uliofanyika mwaka 2023 katika mikoa saba ya Tanzania bara na visiwani ulihusisha mikoa ya Dar es salaam, Mwanza, Dodoma, Mbeya, Arusha na Unguja.

Amefafanua kwambajumla ya kampuni 334 yaliyosajiliwa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) pamoja na Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA) kwa yalifanyiwa utafiti huu.

Latifa ameongeza katika utafiti huo, sekta 10 zilihusika katika ukusanywaji wa takwimu hizo ni kilimo, uvuvi, madini, utalii, viwanda, ujenzi, huduma ya fedha na bima pamoja na biashara za jumla na rejareja.

Ameongeza kwamba utafiti huo utaleta matokeo ambayo yatatumika kama fursa katika kuishauri serikali na wadau mbalimbali wa biashara. 

Kwa upande mwingine Latifa amewapongeza wadau walioshiriki katika zoezi la ukasanyaji takwimu za  utafiti huo wa awali, ambao ni Ofisi ya Takwimu (NBS), BRELA na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Zanzibar(OCGS).

Wadau wengine ni Wakala wa Usajili Mtandao (Ega), Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti (ipsos Tanzania) pamoja na wakuu wa mikoa utafiti ulipofanyikia, huku pongezi za dhati zikienda Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na Tantrade.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...