Na Rahma Khamis Maelezo. 11/3/2024

Baraza la Ushindani halali la Biashara Zanzibar limewataka wafanyabiashara kutumia risiti za Elektronik ili kuingizia Serikali Mapato na kutii sheria.

Akizungumza na Waandishi huko Skuli ya Salim Turk Mpendae Afisa Sheria Muandamizi kutoka katika Baraza hilo Thneyun Mabruok Hassan amesema kuwa maadhimisho ya siku ya mtumiaji wameamua kutoa elimu kwa Waalimu ili wweze kufahamu majukumu na kazi zake.

Amesema elimu hiyo ina lengo la kuwafahamisha Watumiaji kufahamu namna ya kutumia bidhaa bora, kufahamu haki na wajibu wao katika kutumia bidhaa ili kulinda afya zao.

“Sisi kama Taasisi inayoshughulikia kumlinda Mtumiaji tuna haki ya kujua na kufatilia haki zao kupitia taasisi mbalimbali.” Alisema Afisa huyo.

Aidha amesema kuwa katika kuelekea siku ya maadhimusho ya kumlinda mtumiaji wamefanikiwa kutoa Elimu kupitia ngazi ya shehia mbalimbali za Mkoa wa Mjini Magharibi.

Nae Mwalimu Mkuu wa Skuli hiyo Raifa Khamis Ahmed amewataka wafanyabiashara na watumuaji kwa ujumla kuhakikisha wanauza bidhaa iliyo bora kwa watumiaji ili kulinda afya.

Hata hivyo ametoa wito kwa Wananchi kudai na kutoa risiti ya eletronik ili kuondosha malalamiko yanayoweza kujitokeza.

Nao Wanafunzi wa Skuli ya Msingi wamesema kuwa Elimu hiyo itawasaidia Wananchi kuifahamu taasisi hiyo na kuenda kudai haki zao wakati wanapopata matatizo.

" Wafanyabuashara wadogo wadogo wengi tunashindwa kutumia risit ya Eletronik kutokana na gharama kubwa ya kumudu kununulia mashine" Walifahamisha washiriki hao.

Aidha wameliomba Baraza hilo kuzidi kutoa Elimu hiyo kwani wanahitaji elimu zaidi kutokana na Watumiaji waliowengi kutofahamu haki na wajibu wao.

sambamba na kuiomba Serikali kuwachukulia hatua wale wote wanaokwenda kinyume na Sheri zilizowekwa ili waweze kuachana na vitendo hivyo na kumlinda mtumiaji.

Katika kuadhimisha siku ya Mtumiaji ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo marchi 15, Baraza la kumlinda Mtumiaji Zanzibar linashirikiana na Taasisi mbalimbali ikiwemo Kampuni ya Ujenzi Malindi, Kampuni inayoshughulikia mikoop Michenzani,Zanzibar Chemba Of Comas , Maduka ya Madawa pamoja na Skuli ya Salim Turk ili kuweza kutoa Elimu.

Afisa Sheria Baraza la ushindani halali wa Biashara Thneyun  Mabrouk  Hassan akijenga uwelewa kwa  walimu wa skuli ya Salim Turkey juu ya  baraza hilo kuelekea maadhimisho ya siku ya mtumiaji inayoadhimishwa kila ifikapo machi 15 duniani kote.

PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...