*Dkt.Msuya anena mafanikio ya Rais yanakwenda na dhamira ya dhati

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

KAIMU Mkuu wa cha Ufundi Stadi cha Furahika jijini Dar es Salaam, Dkt David Msuya amesema wamejipanga kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan katika nyanja ya elimu kwa kutoa mafunzo kwa fani mbalimbali bure.

Pia amempongeza Rais Samia kwa jitihada kubwa ambazo amezifanya katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi kwa kusimimia vema miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya elimu, afya, barabara kwa kupeleka fedha maeneo hayo ili kuleta tija stahiki kwa watanzania.

“Tangu mwaka 2021 chini ya Serilkali ya Rais Samia tumekuwa tukitoa elimu bure kutokana na ufadhiri tunaoupata kutoka katika mashiriki mbalimbali kwa lengo la kuwasaidia vijana ambao wamepata alama hafifu kidato cha na nne ama walioshia darasa la saba na kushindwa kuendelea na masomo kutoka na hali ngumu za wazazi au walezi wao,” amesema.

Amesema tangu wakati huo vijana 2400 wamefanikiwa kupata elimu ya kozi mbalimbali ikiwemo hoteli, IT, Udereva, umeme, ushonaji na bandari huku wengi wao wakiwa wamepata kazi na wengine wakijiri na kuondokana kwenye dimbwi la umasikini na hali ngumu ya maisha na kujisaidia wao na familia zao.

Chuo hicho chenye namba ya usajili VET/DSM/ PR/ 2021 katika mwaka huu wa masomo ambao unafungwa Mei 26, 24 wanatarajia kusajili vijana 320 kwa kozi mbalimbali na Kaimu Mkuu huyo wa Chuo akitoa wito kwa wazazi nchi nzima kupeleka vijana wao ili wapate elimu bure itakayowasaidia katika maisha yao.

Pia ametoa rai kwa Serikali kuendelea kutoa elimu ya ukosefu wa kinga mwilini (UKIMWI),Unyanyasaji wa kijinsia hususan vijijini ili wananchi waweze kubaliana na changamoto hizo kikamili na si kuishia jijijni Dar es Salaam pekee.

“Wiki iliyopita nilikuwa Namtumbo, ukweli ni kwamba wengi wa wananchi hajui namna na kupambana na unyanyasaji hivyo Serikali ikiongeza nguvu vijijini ukatili utapungua kwa asilimia kubwa,” amesema.

Dkt Msuya ameongeza kuwa kutokana na wengi wa wananchi hususan wanaoishi mikoani imesababishwa watu wenye ulemavu kuchukuliwa na kupelekwa jijini Dar es Salaam na kufanya mtaji kwa kuingizwa katika biashara ya ombamba hivyo ni vema Serikali ikatunga sheria ili kuwadhibiti watu wanaofanya vitendo hivyo ambavyo ni sehemu ya ukatili katika jamii.

Wakati huo huo ametoa pendekezo kwa Serikali kuunda mabaraza ya watoto kwenye shule na wajumbe wao wawe walimu hususan wa kike ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wanapata changamoto ya ukatili kuweza kutoa taarifa bila woga.

Naye Mwanafuzi wa chuo hicho kwa kozi ya kompyuta, Aziza Kusanga ametoa shukrani kwa Rais Samia kwa kukiwezesha chuo cha Furahika kupata ufadhiri ambao umewasaidia vijana kujiendelea kielimu katika programu ya eilimu bure.

Pia mwanafunzi Ramadhani Said, kwa upande wake amesema Rais Samia amekuwa mtetezi kwao baada ya kufanya vibaya kidato cha nne, wamepata fursa nyngine ya kupata ujuzi bure kupitia chuo cha Furahika.
 

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Furahika Dkt.David Msuya akizungumza  na waandishi wa habari  kuhusiana na Chuo hicho kutoa ufadhili wa masomo bure kwa vijana,jijini Dar es Salaam .
 

Kijana wa Kike Aziza Yunus akizungumza  kuhusiana na Chuo cha Furahika kumfadhili bure kusoma kozi ya anayotaka,jijini Dar es Salaam .
 

Ramadhan Said akizungumza kuhusiana na ufadhili wa kusoma bure kwa neema ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika chuo cha Furahika jijini Dar  es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...