Bohari ya Dawa leo imekabidhi bidhaa za afya mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko Wilayani Rufiji mkoani Pwani.

Bidhaa hizo zimekabidhiwa kituo cha Afya Mohoro kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ambazo ni pamoja na Dawa, za kuzuia na kutibu malaria, kuhara na yale ya mlipuko kama vile kipindupindu.

Kwa upnde wa vifaa tiba ni pamoja na magodoro, mashuka na vyandarua, milingoti ya kutundikia maji tiba ( Drip Stand), Binliners na vifaa vingine vitakavyosaidia katika zoezi hili.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa bidhaa hizo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Dr. Hamis Abdallah. ameishukuru MSD kwa juhudi za haraka zilizofanyika kuweza kuwafikia wahanga wa mafuriko. Ameongeza kuwa bidhaa hizo zitasaidia katika utoaji wa huduma kwa waathirika wa mafuriko.

Naye meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam Betia Kaema amesema MSD baada ya kuona taarifa ya janga hili iliamua kuchukua hatua za haraka ikiwemo kuwasiliana na mamlaka za Wilaya ili kufahamu mahitaji yanayotakiwa kwa waathirika. 

“Leo tumekabidhi vifaa ili kuhakikisha huduma za afya hazisimami kwa wananchi, lakini pia tumetembelea maeneo mbalimbali kujionea hathari za mafuriko haya.MSD itaendelea kutoa ushirikiano mpaka pale hali itakapotengamaa." Alisema Betia.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...