Katika kuunga mkono makundi mbalimbali na kurudisha kwa jamii, KCB Bank Tanzania imedhamini na kushiriki mbio fupi za hisani za Run4Autism Tanzania zenye lengo la kuongeza uelewa juu ya tatizo la usonji nchini.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa kama mgeni rasmi, alitoa pongezi za kwa Benki ya KCB Tanzania kwa kuendelea kuunga mkono makundi jitihada mbalimbali kupitia uwekezaji kwa jamii.

Mkuu wa Idara ya Masoko, Uhusiano na Mawasiliano, Christina Manyenye akimuwakilisha Mkurugenzi wa Biashara wa Kanda wa KCB Group na Mkurugenzi Mtendaji wa KCB Bank Tanzania, alisisitiza kuwa mbali na mafunzo ya ujuzi na ufundi ya 2jiajiri, KCB Bank Tanzania itaendelea kutekeleza azma yake ya kuigusa jamii na makundi mbalimbali kwa namna tofauti.

“KCB Bank tunaungana na Lukiza Foundation katika kuleta elimu ili wazazi wengi wajitokeze na kuwasaidia Watoto wenye tatizo la usonji nchini, tunaamini kupitia mbio hizi tunachangia katika kuleta mabadiliko Chanya kwa manufaa ya jamii yetu, alisema.

Kupitia mbio hizi, benki imeonesha dhamira yake ya kuunga mkono jitihada za kuongeza ufahamu wa ugonjwa wa usonji na kuendeleza michezo nchini.

Mbali na hilo, benki ya KCB inashiriki katika masuala mbalimbali ya kimaendeleo ikiwamo kusaidia vijana kielimu na kiujuzi kupitia program ya 2jiajiri ambayo imekuwa chachu katika kupunguza tatizo la ajira.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akimkabidhi cheti cha udhamini Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa KCB Bank Tanzania, Christina Manyenye wakati wa mbio za usonji (Run4Autism Marathon) zilizofanyika siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam.







1. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa na viongozi mbalimbali, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa Masoko, Mawasiliano na Uhusiano wa KCB Bank Tanzania, Christina Manyenye wakati wa mbio za usonji (Run4Autism Marathon) zilizofanyika siku ya Jumapili jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...