NA WILLIUM PAUL, SIHA.

MWENGE wa Uhuru umepokelewa katika wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro ambapo unatarajiwa kuzindua miradi sita yenye thamani ya Bilioni 6.933.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa Mwenge huo ukitokea wilaya ya Hai, Mkuu wa wilaya ya Siha, Dkt. Christopher Timbuka alisema kuwa, Mwenge huo utakimbizwa kilomita 196 kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbali mbali.

Alisema kuwa, Mwenge huo utatembelea darasa la Watoto wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Sanya juu ili kuona namna ambavyo wanafaidika na matunda ya Serikali ya awamu ya sita.

Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa, pia utashuhudia upandaji miti ikiwa ni kumbukumbu ya kutunza mazingira ambapo wilaya hiyo imeshapanda miti mingi katika kipindi hiki cha mvua lengo likiwa ni kutunza mazingira.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...