Na Jane Edward, Arusha

Mkutano wa jukwaa la tatu la usalama wa mtandao umekutana jijini Arusha kufanya tathmini ya utekelezaji na mikakati mbalimbali na kutoa ushauri pamoja na mwelekeo wa Matumizi salama ya mitandao ya kompyuta na huduma za kieletroniki kwa ujumla.

Akizungumza katika Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu Dkt Moses Mwasaga amesema Taasisi ya TEHAMA imeona ni vema wadau wote kukutana ili kujalidili masuala ya kitamtandao jijini Arusha.

Amesema kuwa kufanyika kwa Mkutano huo kunatoa fursa ya kujadili kuhusu mambo ya kimtandao ambapo tume ya TEHAMA ndio wenyeji wa Mkutano huo ambapo utafanyika kwa siku mbili.

"sote tunafahamu kuwa suala la mageuzi ya kidigitali ni endelevu na mtambuka hivyo sote kwa pamoja hatuna budi kuendelea kuchukua hatua za makusudi za kutunga na kusimamia utekelezaji wa sera zitakazolinda usalama wa wadau wote katika ikolojia ya kidigitali"Alisema

Aidha amesema pamoja na uwekezaji mkubwa unaofanywa katika miundombinu ya mawasiliano,ujenzi wa mifumo ya TEHAMA kuendeleza wataalamu na wabunifu hao ili kuhakikisha sera zinachagiza maendeleo ya kidigitali.

Ameongeza kuwa kwa kushirikiana na wizara itaendelea kuchagiza ukuaji wa uchumi wa kidigitali kwa kasi zaidi ambapo 2022 Bunge limepitisha sheria ya ulinzi wa Taarifa binafsi na kwa kupitia sheria hiyo tume imeanzisha tume ya Taarifa binafsi.

Hata hivyo kauli mbiu ya jukwaa hilo ni kutengeneza dunia ya mtandao iliyo jumuishi na shirikishi.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...