Na Karama Kenyunko Michuzi Tv

MAHAKAMA ya Mwanzo Kariakoo jijini Dar es Salaam imemuachia huru Denis Mfumbulwa (44), anayedaiwa kujipatia huduma Serena Hotel kwa njia ya udanganyifu kwa kuwa hakuna ushahidi wa kuthibitisha kuwa kesi hiyo dhidi ya mshtakiwa ni ya jinai.

Uamuzi wa kumuachia mtuhumiwa huyo umetolewa leo Mei 15, 2024 na Hakimu Gladness Njau wakati kesi hiyo ilipoitwa leo mahakamani hapo kwa ajili ya kusikilizwa.

Mapema Meneja wa Hoteli hiyo, Desdery Doto alifika mahakamani hapo kutoa ushahidi ambapo alipoulizwa alidai mshtakiwa alifika hotelini hapo ambapo alikuwa anapata huduma ya chakula na malazi bila kulipa na kutoweka.

Kufuatia maelezo hayo, Hakimu Gladness Njau alimuachia huru mshtakiwa huyo akisema "inaonekana asili ya shauri hili ni la madai na siyo jinai hivyo kama mlalamikaji ataona inafaa afungue kesi ya madai"

Katika kesi hiyo mshtakiwa Mfulumbwa anayeishi Goba Kulangwa anadaiwa kuwa, Machi 6,2022 hadi Machi 28,2024 kwa nyakati tofauti katika Hoteli ya Serena Mtaa wa Ohio Wilaya ya Ilala, Dar es salaam alijipatia huduma ya malazi na chakula yenye thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 21 bila kulipa mali ya Desdery Dotto.

Inadaiwa mshtakiwa baada ya kupatiwa huduma hiyo alitoweka huku akijua kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.

Hata hivyo mpaka sasa mshtakiwa huyo bado yuko mahabusu.

Akizungumza nje ya mahakama Meneja uhusiano huyo amesema yuko tayari kuendelea na kesi ya madai hivyo anasubiri nakala ya hukumu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...