Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekelege Mpulla (kushoto) na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC)  Gilead Teri, wakipeana mikono baada ya kumaliza kusaini mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha kwa haraka migogoro  ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao za ukuzaji uchumi wa nchi. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo Mei 2,2024 jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kulia na kushoto ni wanasheria.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Usekelege Mpulla ( kushoto) na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC)  Gilead Teri, wakisaini mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha kwa haraka migogoro  ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao za ukuzaji uchumi wa nchi. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo Mei 2,2024 jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekelege Mpulla (kushoto) na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC)  Gilead Teri, wakibadilisana mikataba mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha kwa haraka migogoro  ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao za ukuzaji uchumi wa nchi. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo Mei 2,2024 jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia kulia na kushoto ni wanasheria.
Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji  Tanzania (TIC)  Gilead Teri akizungumza wakati wa hafla ya kusaini  mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha kwa haraka migogoro  ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao za ukuzaji uchumi wa nchi. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo Mei 2,2024 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Usekelege Mpulla akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha kwa haraka migogoro  ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao za ukuzaji uchumi wa nchi. Hafla ya makubaliano hayo imefanyika leo Mei 2,2024 jijini Dar es Salaam.

KATIKA kuhakikisha mazingira bora kwa wawekezaji nchini Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) wamesaini makubaliano ya kufanya kazi kwa pamoja ili kusuluhisha haraka migogoro ya kazi na kuruhusu wawekezaji kufanya kazi zao ukuzaji uchumi

Makubaliano hayo yamesainiwa leo Mei 2, 2024 na pande zote mbili huku upande wa TIC ukiwakilishwa na Mkurugenzi wake Mtendaji Gilead Teri na upande wa CMA ukiwakilishwa na Mkurugenzi Mkuu wake Usekelege Mpulla huku wakurugenzi hao wote wakikiri kuwa hilo ni gaizo la Rais Samia Suluhu Hassan

Teri amesema kuwa Taasisi hizo zimeungana kuhakikisha mwekezaji anapata mazingira mazuri ya kufanya shughuli zake.

"Naomba nieleweke kuwa sio wawekezaji wa nje tu wanaopata changamoto hata wa hapa ndani hivyo tunatekeleza agizo la Rais juu ya kuhakikisha wawekezaji wanapotaka kuwekeza wafanye kazi zao kwa misingi ya sheria pasipokuwa na uonevu".

"Palikuwepo na hisia kwamba baadhi ya mifumo na sheria zinatoa mianya kwa baddhi ya wawekezaji kuonewa eneo moja wapo katika utatuzi na usuluhishi wa migogoro kati ya wawekezaji na waajiriwa" amesema Teri.

Ametanabaisha kuwa jitihada hizo hazikufanywa na TIC isipokuwa ni msukumo wa Mkurugenzi wa CMA , Mpulla ambaye alifika TIC kwa ajili ya kujadili nia ya kumaliza tatizo hilo.

"Jitahada hizi zimetoka kwa ndugu yangu Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), na yeye ndiye aliyetutafuta akisema hatutaki wawekezaji wenu wakija suala la usuluhishi liwe changamoto kwao wakija kuwekeza, naomba nikupongeze sana ndugu yangu, wewe pamoja na timu yako yote kwa kuona umuhimu wa kushirikiana na TIC ili kuhakikisha kwamba mazingira ya uwekezaji nchini yanakuwa rafiki" amesema Teri.

Amesema kuwa Taasisi hizo zimekubaliana mambo mengi lakini mambo mawili ndio msingi tumekubaliana mambo mengi lakini ya msingi niol mawili.

"Jambo la kwanza tulilokubaliana kushirikiana CMA na TIC ni kukuza uelewa wa masula ya usuluhishi na uamuzi wa migogoro ya watumishi au wafanyakazi tungependa wawekezaji wote wafahamu sheria za hapa nchini , haki zao na wajibu wao kwenye eneo hili tutahakikisha kila mwekezaji anazijua "

"Eneo la pili ni kukuza majadiliano katia ya wewekezaji kaytia CMA, TIC na wawakilishi wa Wafanyakazi lengo lake kabla changamoto zikafika hatua mwekezaji hajapigwa faini kubwa kuwe na namna ya majadiliano kwa pamoja katia ya CMA na TIC bila kuathiri sheria zote mbili." amesema Teri.

Teri amesema Taasisi hizo zinatekeleza adhma ya rais mwekezaji yoyote awe wa ndani au kutoka nje asikutane na vikwazo vitakavyomrejesha nyuma kwenye uwekezaji wake muhimu umma ufahamu uwekazaji na ajira ni pande mbili za sarafu moja pakitokea uwekezaji wanafaika namba moja ni Watanzania wanaoajiriwa.

Kwa upande wake, Mpulla amesema kuwa CMA imebeba jukumu hilo ili kupunguza msongamano wa mashauri ya migogoro kazini "tulijiona tunawajibu wa kuunga mkono juhudu za Rais kwenye kuvutia uwekezaji nchini tumeona anakwenda huku na kule kuwavuta waje sasa hawa wanaokuja sisi tunawajibu wa kuwahuduma vizuri ili waambiane waje": .

"Majukumu yetu makuu ni utatuzi wa migogoro ya kazi kwa njia ya usuluhishi na uamuzi tunajukumu la kisheria na kwamba sheria ya ajira na mahusiano kazini lengo kuu ni kuchochea ukuaji wa uchumi kupitia haki jamii kama kuchochea ukuaji wa uchumi na wenzetu TIC wanamalengo hayo hayo kwa hivyo hiyo ndio sababu ya kuungana nao" Amesema Mapulla.

Mapulla amesema uwekezaji unachochea ajira ilhali ajira zinakuwa zinamigogoro "Kadri wawekezaji wanavyokuja nchini ndivyo fursa za ajira zinavyoongezeka kadri fursa hizo zinavyoongezeka basi uwezekano wa kutokea migogoro ya kikazi ni mkubwa na sisi tunapaswa kuingia hapo kumhakikishia mwekezaji kwamba iwapo itatokea migogoro yab kikazi katika nchi yetu basi MCA tutahakikisha tunatengeneza amani sehemu ya kazi kwa hivyo tunawajibu wa kuwahakikishia wawekezaji kuwa migogoro inatatuliwa kwa wakati na kwa haki na kuhakikisha wanatumia muda mwingi kuzalisha na kukuza uchumi kuliko kutumia muda mwingi kwenye migogoro" amesema .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...