MATUMIZI ya njia mbalimbali za uzazi wa mpango yameongezeka katika Zahanati ya Ubinga Kijiji cha Ubinga wilayani Nzega mkoani Tabora ambapo kwa wiki wanahudumia wahitaji 100 kutoka 40 kwa mwaka 2021.

Wakati kukiwa na ongezeko hilo, mkakati wa serikali kupitia Wizara ya Afya katika matumizi ya uzazi wa mpango kwa mwaka 2019/2023 ulikuwa unakadiriwa kupunguza mimba zisizotarajiwa 7,148,748, utoaji mimba holela 2,669,638 na vifo 22,164.

Ongezeko hilo la matumizi ya uzazi wa mpango katika kijiji hicho cha Ubinga umetokana na uhamasishaji uliofanywa na Shirika lisilo la Kiserikali la Maria Stopes Tanzania kupitia mradi wake wa kuimarisha vituo vya umma (Public Sector Streghtening-PSS ) kuwawezesha wahudumu wa afya kupata elimu na kuwajengea uwezo na kuwezesha upatikanaji wa njia za uzazi wa mpango.

Akizungumza na Michuzi Blog, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Ubinga, Raphael Peter amesema mafunzo yaliyotolewa na Maria Stopes kupitia mradi wake wa PSS yameleta tija kwa jamii yao.

Amesema, tangu wahudumu wapate mafunzo ya utoaji huduma ta uzazi wa mpango na kuwezeshwa vifaa, huduma hizo zimekuwa zikifanyika kila siku katika zahanati hiyo tofauti na hapo mwanzo ambapo huduma zilifanyika mara moja kwa mwezi.

“Siku za nyuma huduma hizi hazikutolewa kwasababu watoa huduma walikuwa hawana ujuzi huu vizuri, kwahiyo tulianza kuhamasisha kupitia wahudumu wetu waliopo kwenye jamii wateja wakaanza kuongezeka namba iliongezeka na zaidi namba hiyo inajieleza kwenye vitabu kulingana na takwimu zilizopo kwenye mifumo ya afya” amesema Dk Peter

Amesema kituo cha Ubinga kimenufaika kwa kiwango kikubwa kwa kupata vitendea kazi vya mara kwa mara na kutembelewa na wadau wengi hivyo kufanya huduma za uzazi wa mpango kuwa hai huku akitaja changamoto kubwa kuwa ni kuwa na muitikio mdogo kwa upande wa akina baba.

Kwa upande wake Muuguzi na Mkunga katika zahanati ya Ubinga Aziza Simangwa amesema kumekuwa na changamoto kubwa ya imani potofu ambapo zinaletwa na maneno ya mtaani na kupotosha watu kuhusu matumuzi ya uzazi wa mpango.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...