Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mazingira na Nishati wa Uingereza Mhe. Lord Benyon jijini Paris nchini Ufaransa leo tarehe 14 Mei, 2024.

Kikao hicho kimefanyika kando ya Mkutano wa Nishati Safi ya Kupikia ambao Mwenyekiti Mwenza ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika kikao hicho, Waziri Dkt. Jafo na Waziri Benyon Mawaziri hao wamejadili mambo mbalimbali yakiwemo ya nishati safi ya kupikia.

Halikadhalika, masuala ya miradi itakayohusu uchumi wa bluu nchini Tanzania yamejadiliwa na viongozi hao.

Hivyo, Uingereza imeahidi kuisaidia Tanzania katika maeneo hayo mawili ambayo yataleta tija katika hifadhi ya mazingira.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme na Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira) Bi. Kemilembe Mutasa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akifanya mazungumzo na Waziri wa Mazingira na Nishati wa Uingereza Mhe. Lord Benyon jijini Paris nchini Ufaransa leo tarehe 14 Mei, 2024, Kikao hicho kimefanyika kando ya Mkutano wa Nishati Safi ya Kupikia ambao Mwenyekiti Mwenza ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mazingira na Nishati wa Uingereza Mhe. Lord Benyon (wa pili kushoto) mara baada ya kufanya kikao jijini Paris nchini Ufaransa leo tarehe 14 Mei, 2024, kando ya Mkutano wa Nishati Safi ya Kupikia ambao Mwenyekiti Mwenza ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Wengine wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme na kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira) Bi. Kemilembe Mutasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...