Na Mwandishi Wetu
MFUKO binafsi wa kusaidia wakulima PASS Trust kwa kushirikiana na Ubalozi wa Denimark wamezindua na kukabidhi kituo atamizi cha vijana cha ufugaji biashara kwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi chenye thamani ya Sh.bilioni 1.63.
Hafla hiyo ya ufunguzi na makabidhiano imefanyika leo Mei 14,2024 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega pamoja na viongozi kutoka katika wizara nyingine.
PASS Trust imeamua kukabidhi umiliki wa kituo hicho kwa Taliri, kufuatia makubaliano baina ya pande hizi mbili ambayo yalifanyika mwaka 2018 wakati kituo hicho kikianzishwa. Kituo hiki kwa sasa kitasaidia kuwainua vijana wa Kitanzania, kupitia program atamizi chini ya Wizara ya mifugo na Uvuvi.
Mradi huo utaleta mabadiliko chanya hasa katika sekta ya ufugaji, kwa kuwakusanya vijana na kuwapa ujuzi na maarifa ya unenrpeshaji mbuzi sambamba na ujasiriamali katika mnyororo mzima wa ufugaji Biashara.
Hiyo itasaidia vijana kuweza kujiajiri, kuweza kuyafikia masoko ya nyama pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa malighafi za viwanda vya nyama ili kutanua soko la nyama kimataifa
Akizungumzia mradi huo wa kituo atamizi cha ufugaji biashara cha vijana, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa asilimia 67 ya nguvu kazi ya taifa ni Vijana. Hivyo uwepo wa miradi ya namna hii unasaidia kuleta manadiliko chanya kwa wafugaji wadogo.
Ameongeza kuwa kupitia miradi hii serikali imeweza kutanua wigo wa masoko ya nyama kimataifa ili wafugaji waweze kunufaika na masoko hayo.
Ameongeza kuwa “usafirishaji wa nyama kimataifa umeongezeka kwa kiasi kikubwa na kufikia toni 11682.3, ikiwa ni pamoja na tani za nyama 870.7, tani 8059.48 za nyama ya mbuzi,tani 27.5 za nyama ya kondoo,na tani 9.3 za nyama ya nguruwe.Tani hiz zote zimeuzwa kwa thamani ba bilioni 50.3 kufika mwezi aprili Mwaka huu”.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano Charles Chiza Sylivia ambaye ni Mjumbe wa bodi wa PASS Trust akimuwakilisha Mwenyekiti wa bodi ya PASS Trust amesisitiza wamekuwa tukitumia vituo hivyo atamizi vya kilimo biashara kutoa mafunzo, na kuongeza weledi kwa vijana wa Taifa letu.
"Tunajivunia mafanikio haya ambayo tangu mwaka 2019 zaidi ya vijana 30 wameweza kunufaika na mradi huu wa Kngwa na wameweza kuanzisha miradi yao sehemu mbalimbali hapa nchini."
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...