Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akiwa pamoja na wajumbe  kutoka Wizara zinazohusika na Masuala ya Kilimo, Maji, Nishati na Uratibu wa Udhibiti wa Maafa wa nchini Tanzania wakati wa Mkutano wa kujadili hali na athari za mvua za El Nino katika Ukanda wa SADC uliofanyika kwa njia ya mtandao Jijini Dodoma.


NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama ameshiriki katika Mkutano wa kujadili hali na athari za mvua za El Nino katika Ukanda wa SADC.

Mkutano huo ulifanyika  kwa njia ya Mtandao (Zoom meeting)   tarehe 14 Mei, 2024 Jijini Dodoma ukihusisha Wizara za Kisekta  zinazohusika na Masuala ya Kilimo, Maji, Nishati na Uratibu wa udhibiti wa Maafa ni maandalizi ya Mkutano wa dharura wa Wakuu  wa Nchi na Serikali  wa Jumuiya ya Maendeleo ya  Kusini mwa Afrika (SADC) Kuhusu Hali ya Mvua za El nino utakaofanyika kwa njia ya Mtandao Mei 20, 2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...