Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema Muhimbili itaendelea kuwajengea uwezo wataalam wake kwakuwa malengo yaliyopo kwa sasa ni kuifanya Muhimbili Mloganzila kuwa kituo kikubwa cha umahiri katika huduma za upasuaji rekebishi katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

Prof. Janabi amesema hayo alipokutana na timu ya wataalam wa upasuaji kwa lengo la kuwashukuru na kuwapongeza kwa kufanikisha kambi ya upasuaji rekebishi iliyofanyika hivi karibuni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila , ambapo kambi hiyo ilishirikisha wataalamu kutoka MNH Upanga Mloganzila, MUHAS pamoja na mtaalamu mbobezi kutoka nchini India.

Akizungumzia kuhusu upasuaji huo Prof. Janabi ameeleza kuwa hadi sasa idadi ya wagonjwa waliofanyiwa upasuaji wa kupunguza uzito wamefikia 187 na kati ya hao asilimia 80 wamefanyiwa upasuji wa mfumo wa chakula.

“Tumewafanyia upasuji kwa makundi matatu, kuna waliowekewa puto tumboni, wengine wamepunguzwa ukubwa wa tumbo na baadhi wamefanyiwa upasuaji wa kunyonya mafuta”amesema Prof. Janabi.

Prof. Janabi ameongeza kuwa tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo imekuwa na matokeo chanya ambapo kuna baadhi ya wagonjwa ambao walipata maradhi ya kisukari kilicho sababishwa na uzito mkubwa ila baada ya kufanyiwa upasuaji afya zao zimeanza kuimarika.

“Mbali ya kuwafanyia upasuaji, wamewapatiwa elimu ya chakula na wameweza kubadilisha mtindo wao wa maisha, sasa wanakula chakula kidogo jambo ambalo linawasaidia kuthibiti hali ya sukari mwilini”amesema Prof. Janabi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...