Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amekutana na kufanya mazungumzo na wataalam kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania kwa lengo la kujadiliana na kuangalia eneo maalum litakalofaa kwa ajili ya kushuka helikopta zitakazo leta wagonjwa watakaokuja kutibiwa hospitalini hapo.

Kwa mujibu wa Prof. Janabi Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila ni hospitali ya kisasa yenye miundombinu rafiki na kuongeza kwamba Muhimbili ni Hospitali ya Taifa hivyo ni muhimu kuwa na eneo kama hilo ili ikitokea wagonjwa wanaohitaji huduma za dharura kunakuwepo na mazingira rafiki zaidi ya kufika hospitalini ukilinganisha na kutumia usafiri wa barabara.

“Eneo ambalo lilikuwa linatumika Muhimbili kwasasa si rafiki kutokana kuwa na majengo marefu hivyo wataalamu hao wameona ni vema wakafika MNH Mloganzila ili kuona mazingira na kisha kufanya maamuzi na hatimaye kutengeneza eneo maalumu la kushukia helikopta.” amesema Prof. Janabi

Kwa upande wake Bw. Pius kazeze ambaye pia ni Meneja Uendeshaji Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere amesema wameridhika na eneo ambalo wameliona kwani ni kubwa na linafaa ingawa kuna vitu vya kitaalam ambavyo vitafanyiwa kazi.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...