NA VICTOR MASANGU,KIBAHA

JESHI la Polisi Mkoa Pwani limewaonya vikali baadhi ya madereva wa Bodaboda kuacha kabisa na kuingilia misafara ya viongozi waandamizi na badala yake wanapaswa kuiheshumu pindi inapopita ili kuweza kuepukana na ajali ambazo zinaweza kupelekea watu kujeruhiwa vibaya na kupoteza maisha yao.

Onyo hilo limetolewa na Kamanda wa Polisi mkoani Pwani Pius Lutumo wakati Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Kampuni ya Priamid oil walipotoa Elimu ya usalama barabarani sambamba na uzinduzi rasmi wa kituo ha mafuta kilichopo eneo la kwa Mbonde mkoani Pwani

Kamanda Lutumo alisema kwamba madereva wa boda boda wanapaswa kuweka misingi ya kuheshimu misafara ya viongozi waandamizi ikiwa sambamba na kuzingatia sheria mbali mbali za barabarani.

Aidha Kamanda Lutumo aliwapongeza wawekezaji wa kiwanda hicho cha Pyramid Oil kwa kuamua kukijenga katika eneo la Kibaha ambalo kwa sasa lina viwanda mbali mbali ni moja ya hatua ya kuleta chachu ya maendeleo.

Kwa upande Kaimu Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Pwani Miraj Mkojera amewataka bodaboda hao kuachana kabisa na tabia ya kubeba mishikaki na kuwahimiza kuvaa kofia ngumu ili kujilinda pindi ajali inapotokea.

Naye mmoja wa wawekezaji ambaye pia ni mkurugenzi wa kituo hicho cha mafuta cha Piramid Victor Betram amempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwawekea mazingira mazuri ya uwekezaji.

Mkurugenzi huyo alifafanua kwamba uwezezaji huo wa kituo cha mafuta umeweza kuwapa fursa mbali mbali za ajira kwa wakazi kutoka Wilaya ya Kibaha kwa kiwango cha asilimia mia moja.

Pia Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba kituo hicho ambacho kimefunguliwa rasmi kimeshatoa fursa za ajira zaidi ya 15 na kwamba kitaendelea kutoa ajira kadiri ya mahitaji.

Nao baadhi ya madereva wa bodaboda ambao wamehudhuria katika halfa hiyo wameahidi kutekeleza maagizo na maelekezo yote ambayo yametolewa na jeshi la Polisi.

Kadhalika walisema ujio wa mradi huo wa kituo cha mafuta utaweza kuwasaidia kuondokana na kwenda kutafuta huduma ya mafuta katika eneo la mbali na kudai kwao ni mkombozi mkubwa.

Katika halfa ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho cha mafuta pia kulitolewa mafunzo mbali mbali kwa madereva wa boda boda kutoka kwa jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani lengo ikiwa ni kuwakumbusha kuzingatia sheria za barabarani bila kushurutishwa.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...