Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima amewataka wanahabari kuwa mabalozi wa utalii, kuandika taarifa zinazowavutia watalii kutoka nje na ndani ya nchi.

RC Malima ameyasema hayo wakati akifungua Mafunzo kwa wanahabari yaliyoandaliwa na Chama Cha Waandishi wa habari Tanzania (TAMPA) kwa kushirikiana na TANAPA ambapo amesema Mkoa wa Morogoro unahifadhi Tatu Kubwa ambazo ni Mikumi,Udzungwa na Mwalimu Nyerere zenye vivutio kadha wa kadha huku vingine vikiwa havipatikani mahala popote Duniani

Katika kutoa fursa kwa watalii kuweza kufika kwa urahisi katika hifadhi ya Taifa Mikumi serikali ina mpango kufungua geti Kilosa kuingia Hifadhi hiyo kutokana na kuwepo Kwa treni ya mwendokasi.

Kwa Sasa watalii wanalazimika kusafiri zaidi ya kilometa 100 kutoka kilosa Hadi Mikumi na endapo geti Hilo litafunguliwa watasafiri kilometa 15 kuingia hifadhini.

Hifadhi ya Mikumi inafikika kwa urahisi kwa kutumia njia mbalimbali ambazo ni barabara ya TAZAM, Reli ya kati na Reli ya SGR na njia ya anga hivyo watalii wanapata fursa ya kuona wanyama kirahisi.

Aidha RC Malima amewataka wadau mbalimbali kuanza kujenga hoteli nzuri zenye viwango katika maeneo mbalimbali ikiwemo Kisaki Ili kuhudumia watalii wanaotembelea hifadhi ya Mwalimu Nyerere, Mikumi, Doma Kwa hifadhi ya Mikumi na Ruaha kwa hifadhi ya Udzungwa.

Akizungumza katika mafunzo hayo Rais wa TAMPA, Simon Mkina amesema lengo la semina hiyo ni kuwaandaa wanabari kuwa sehemu ya utalii Kwa kushiriki moja kwa moja Ili kutimiza malengo ya Serikali kupitia filamu ya THE ROYAL TOUR huku Katibu wa MOROGORO PRESS CLUB Lilian Kasenene amesema mafunzo hayo yametolewa muda muafaka ambapo ameahidi Chama cha waandishi wa habari Morogoro kupitia wanachama wake kitakuwa mstati wa mbel katika kitangaza utalii,

Naye Mkufunzi Mwanadamizi Chuo cha Taifa cha Utalii Agapiti Roman amesena mwaka 2023 jumla ya watalii Milioni 1.8 walitembelea Hifadhi za Taifa nchini kutoka Mili. 1.3 mwaka 2022 na hii ni niongezeko kubwa baada ya filamu ya THE ROYAL TOUR ambayo imekua chahu kubwa kwa nchi.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...