a Said Mwishehe, Michuzi TV

SERIKALI kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema tayari imeweka mipango mkakati inayohakikisha kunapatikana rasilimali watu yenye ubunifu na itakayoendana na sayansi na teknolojia.

Katika kufanikisha hilo imesema ipo kwa sasa wapo hatua ya kuainisha mahitaji, sifa na aina ya teknolojia zinazohitajika katika sekta mbalimbali na kuweka muda maalum kwa ajili ya kupatikana ili kuendana na kasi ya ukuaji wa Teknolojia kwa maendeleo ya nchi yetu.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliohusisha wadau mbalimbali wa masuala ya ubunifu wakiwemo Wahariri wa vyombo vya habari ,Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Ladislaus Mnyone amesisitiza Serikali inatambua umuhimu wa kukuza na kuendelea bunifu mbalimbali.

Profesa Mnyone aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao hicho kuelekea maadhimisho ya miaka 10 ya Wiki ya Ubunifu inayoanza kesho amesema Serikali inalenga kuhakikisha sayansi na teknolojia inapewa kipaumbele katika maendeleo ya rasilimali watu na ubunifu.

Amefafanua kwamba maandalizi ya mpango wa taifa wa teknolojia utasaidia nchi na wadau kuwekeza katika maeneo ambayo Serikali itakuwa imeyaainisha huku akifafanua hata mabadiliko ya mitaala inalenga katika kufanikisha malengo hayo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa COSTECH Dk.Amos Nungu, akizungumzia Wiki ya Ubunifu amesema inaaanza kesho jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julias Nyerere (JNICC) na kilele chake kikitarajiwa kufanyika mkoa wa Tanga.

"Wiki ya wiki ubunifu itaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa wiki ya Ubunifu na kwa mwaka huu kauli mbiu inasema ubunifu kwa maendeleo jumuishi ya rasilimali watu".

Pia amesema kuelekea wiki ya ubunifu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na wadau wa maendeleo wanajivunia hatua mbalimbali ambazo zimepigwa katika ubunifu.

Kwa upande Meneja Progaramu wa Umoja wa Ulaya Janeth Martoo amefafanua kwamba ubunifu unahitajika zaidi kwani unasaidia katika kukuza ustawi wa uchumi wa taifa.

Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Limited (MCL), Bakari Machumu amesema ili kufanikiwa kwa mipango hiyo mchango wa vyombo vya habari inahitajika

"Ili kuyafikia mlengo hayo, unahitaji mchango wa vyombo vya habari, katika kuelimisha, kuibua na kuandika habari zitakazoshawishi umma kuvutiwa na ubunifu,"amesema na kusisitiza ni umuhimu wanaharo kujenga ubobevu katika teknolojia na ubunifu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...