Na Mary Margwe, Simanjiro

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara Mhandisi Joanes Martine amesema Taasisi nyingi Wilayani humo zinadaiwa Ankara za Maji, ambapo hadi kufikia mwezi Machi, 2024 zinadaiwa jumla ya sh.mil.11,702,400,00.

Akizungumza wakati wa kuwasilisa taarifa ya Utekelezaji wa RUWASA Kwa kipindi Cha robo ya tatu Januari -Machi kwenye baraza la Madiwani chini ya Mwenyekiti wake Mh Baraka Kanunga, Meneja wa RUWASA Wilaya hiyo Mhandisi Joanes Martine amesema taarifa hiyo ni ya miradi ya Maji Kwa kipindi Cha miezi hiyo mitatu.

Mhandisi Martine amesema kutokana na deni hilo kwa Taasisi hizo, Ofisi yake imeendelea kutoa elimu na msisitizo Kwa Taasisi kuhakikisha zinalipa madeni yao na kuweka makubaliano ya kuanza kupunguza deni Kwa kipindi kitakachokubalika kabla ya kusitisha huduma.

Licha ya kuwepo kwa deni hilo Kwa Taasisi pia Mhandisi Martine amebainisha changamoto zingine wanazokabiliana nazo kuwa ni pamoja baadhi ya viongozi wa Kijiji kugomea / kukwamisha uunganishwaji wa vyombo vya watoa huduma ya Maji na kupelekea makusanyo kutokufanyika Kwa kutumia mifumo wa GePG.

" Mvua inayoendelea kunyesha kusababisha uharibifu wa Miundombinu ya Maji na maeneo Mengine ya vyanzo vya maji kutokuweza kufikia kiurahisi mfano mradi w Maji Ngage, hizi ndio Miongoni mwa changamoto zinazowakabili " ameongeza Mhandisi Martine.

Awali Mhandisi Martine amesema RUWASA Wilaya ya Simanjiro inatoa huduma katika kata 12 zenye Vijiji 45, ambapo inahudumia asilimia 72.6 ya Wakazi wote ndani ya Wilaya.

" Kata ya Shambarai, Mirerani na Endiamtu zinahudumiwa na Mamlaka ya Maji Arusha na Kata za Orkesument, Endonyong na Langai zinahudumiwa na Mamlaka ya Maji Orkesument " amesema Meneja Martine.

Aidha amefafanua kuwa pamoja na shughuli mbalimbali zinazofanywa na RUWASA Wilayani humo lakini pia katika kipindi Cha mwezi Januari -Machi, 2024, RUWASA imeendelea na ujenzi wa miradi katika Vijiji mbalimbali kupitia Program endelevu wa usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini ( Sustainable Rural Water Supply and Sanitation Program -PforR) Fedha za mfuko wa Maji wa Taifa na fedha zawadau wa Maendeleo.
Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...