Na Mwandishi Wetu


BUNGE  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia  kwa kishindo na kwa asilimia mia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Maji yenye jumla ya Shilingi 627,778,338,000 ili kwenda kutekeleza kazi na shughuli mbalimbali za Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025.

Waziri wa Maji Jumaa Aweso (Mb) akichangia hoja hiyo kabla ya kupitishwa Bungeni amesema Wizara ya Maji imejipanga kuwa mfano kwa Tanzania kwa kutafuta vyanzo vingine vya fedha ili kuwahudumia wananchi.

Ametolewa mfano wa Hatifungani ya Kijani iliyofanikiwa kwa kiwango kikubwa kupitia Mamlaka ya Majisafi Tanga (Tanga UWASA).

Waziri Aweso ameweka wazi kuwa Wizara ya Maji ilikuwa eneo la malalamiko na kero ila hivi sasa ni neema akisema miradi ya maji iliyokwama tangu miaka ya 70 hivi sasa imekamilishwa na wananchi wanapata huduma ya maji.

 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...