Na Ashura Mohamed -Arusha

Serikali imeshauriwa kuboresha miundo mbinu ya Barabara ndani ya hifadhi za Taifa Ili kuwezesha waongoza watalii kufanya kazi katika Mazingira mazuri.

Rai hiyo imetolewa na Mlezi wa Chama Cha Waongoza Watalii Kanda ya Kaskazini yaani Northern Tanzania Safari Guides Society (NTSGS),Bw.Frank Mwaisumbe wakati akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho Uliofanyika katika Chuo Cha Utalii Arusha.

Bw.Mwaisumbe alisema kuwa changamoto ya miundo mbinu ndani ya hifadhi nyingi ni vizuri ikaendelea kuboreshwa ili kuweka mazingira mazuri ya kufurahia madhari kwa wageni ambao wanatoka nje ya nchi.

"Pamoja na Juhudi kubwa nzuri zinazofanyika na serikali ya Awamu Sita chini ya Raisi dkt.Samia Suluhu Hassan kwamba amefanya kazi nzuri ya kuvutia wawekezaji wa kitalii katika ukanda wa Kaskazini na nchini kwa Ujumla lakini pia amefanya kazi kubwa sana ya kuvuta watalii kwa kiasi kikubwa lakini pamoja na hayo bado kumekuwa na changamoto nyingine za miundo mbinu haswa upande wa barabara na sehemu chache zilizopo katika maeneo ya utalii kama sehemu za kupumzika wageni ,sehemu za kutembea wageni ni chache,hivyo wadau wanaiomba serikali kupitia Menejimenti ya Ngorongoro miundombinu hiyo iongezwe ili kuweza kupata nafasi ya Watalii wasitembee umbali mrefu bila kupumzika kuelekea sehemu ambayo wanatakiwa kufika"Alisisitiza Mwaisumbe

Aidha alisema kuwa kumekuwepo na mvua nyingi kupitia kiasi ambazo zimeharibu miundombinu mbinu,hivyo kuiomba Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro kuwa na njia mbadala ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kwa barabara mpya ili kupunguza msongamano.

Ukanda wa Kaskazini ni ukanda ambao unawingi wa vivutio vya Utalii ambao unaiwezesha serikali kukusanya Mapato.

Nae Emmanuel James Matalika ambaye ni Mwenyekiti wa Nidhamu (NTSGS) alisema kuwa kumekuwepo na uchafuzi mkubwa wa Mazingira pembezoni mwa barabara ambao umekuwa ukisababishwa na magari ya abiria kutokana abiria magari hayo kutokuwa na vibebea taka hivyo kusababisha uchafuzi kuendelea kuwepo katika maeneo mbalimbali.

"Kumekuwepo na wasimamizi wengi wa Mazingira ndani ya Jamii lakini bado udhibiti wa taka hizo ni mdogo pembezoni mwa barabara Hali ambayo inaleta shida pindi tunapokuwa na wageni kutoka nje ya nchi wakitoa malalamiko yao juu ya kuzagaa kwa taka ngumu za plastiki jambo ambalo halileti taswira Nzuri Kwa nchi yetu na hatufurahii hali hii kabisa."Alisema bwana Matalika

Pia alisema kuwa wadau mbali mbali wanaojihusisha na swala la Mazingira wahakikishe wanaongeza nguvu ya kuhakikisha mazingira yanakuwa safi huku akiitaka serikali kuingiza Somo la Usafi liwe ni Moja ya somo katika shule za Msingi.

Kwa upande wake Afisa Utalii daraja la Kwanza bw.Fred Baraka Sam kutoka Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro alisema kuwa NCAA inaendelea na maboresho ya miundombinu mbinu haswa barabara,uk
izingatia mvua kubwa zilizonyesha hapa nchini Ili kuhakikisha kuwa Barabara ndani ya hifadhi zinapitia muda wote.

Hata hivyo alisema kuwa NCAA inaendelea na maboresho mengine ikiwa ni pamoja na kuongeza maeneo ya wageni kula chakula na kupumzika (Picnic site's),maeneo ya kulala (Camping sites),ambapo wahandisi na wakandarasi wanafanya kazi usiku na mchana Ili kuweka mazingira kuwa Bora ndani ya mamalaka ya hifadhi ya Ngorongoro na kuendelea kuvutia wageni zaidi.

"Mfano katika upande wa barabara ambao ndio tunazungukia mfano kreta, kutokana na changamoto kubwa ya mvua lakini madereva wa kwetu idara ya uhandisi,udereva wanaendelea na maboresho na matengenezo hadi nyakati za kwa ajili ya kurekebisha maeneo yaweze kupitika kirahisi mfano mzuri ukanda wa round table barabara inapitika vizuri mana ilinyanyuliwa juu. "Alisema Sam

Kabla ya Mkutano Mkuu Waongoza Watalii hao (Guides),Walipata fursa ya kufanya Mafunzo ya siku mbili,Kufanya Usafi wa Mazingira katika barabara ya Arusha mjini hadi Makuyuni na kufuatiwa na Mkutano mkuu wa Mwaka wa Kuchagua viongozi mbalimbali wa Chama hicho.

Baadhi ya Waongoza Watalii ambao ni wanachama wa Chama Cha Waongoza Watalii Kanda ya Kaskazini Wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza Mkutano mkuu ambao ulitanguliwa na Mafunzo  Maalum.

Mmoja wa Viongozi wa chama Cha NTSGS bwana Emmanuel Matalika akizungumza na Vyombo vya habari
Pichani ni Afisa Utalii Daraja la kwanza bwana Fred Baraka Sam kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA)






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...