Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma
Naibu Waziri Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mhe Dkt Festo Dugange amesema kuwa Lishe ni kila kitu katika maisha ya mwanandamu kwani unaweza kuwa na Daktari bora,Mwanasheria bora na Kiongozi bora kama tu amepata lishe bora wakati wa utoto ma kuweza kupata maendeleo ya akili yake vizuri kwani ndipo ataweza kusimamia majukumu vizuri.
Naibu Waziri Dkt Dugange ameyasema hayo mapema Leo Jijini Dodoma Jyly 16,2024 katika ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa uratibu kwa Maafisa Lishe wa Mikoa na Halmashauri Nchini ambao ulikuwa na tukio mahsusi la Uzinduzi wa Makala ya Lishe.
Na kuongeza kuwa kama mtoto hatapata lishe iliyobora utotoni basi italeta athari katika utu uzima wake hasa katika majukumu na kupelekea uzito katika maamuzi na utendaji wake hata kama ni kitu cha kufanya kwa muda mfupi.
"Lishe ni kila kitu,utakuwa na Afisa bora,Mwanasheria bora,utakuwa na Daktari bora,Injinia bora,kutakuwa nna Kiongozi bora kama amepata lishe bora wakati wa utoto na ameweza kuwa na maendeleo ya akili yake vizuri na ndipo ataweza kusimamia majukumu yake vizuri kama amepata lishe bora".
Sambamba na hayo pia amesema kuwa Serikali itaendelea kutenga Bajeti na kutoa vibali kwaajili ajira sambamba na uboreshaji wa changamoto zinazohusu masuala ya muundo wa Utumishi wa kada ya Afya.
Pamoja na hayo Mh Dkt Dugange hakuacha kuwakumbusha Maafisa lishe hao katika kushiriki uchaguzi ujao hivi karibuni na pia kuwaasa kuhamasisha jamii kuhusu matumizi ya Nishati safi kwani ni ajenda ya Taifa.
"Napenda nichukue wasaa huu niwakumbushe mambo makuu mawili,moja kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika baadae mwaka huu tusijitenge na zoezi hilo kwani ni zoezi muhimu na ni la kwetu".
"Pili kuwataka muhamasishe jamii zetu ili zianze kutumia nishati safi ili kuondokana na matumizi ya kuni na mkaa unaoatokana na miti ili kuendelea kutunza mazingira kwani hii ni ajenda ya Kitaifa ya Nishati safi ".
Naye Bi Neema Joshua ambaye ni Mkurugenzi msaidizi Wizara ya Afya Idara ya lishe akitoa salamu za Wizara amesema kuwa Wizara inayajua yote wanayopitia Maafisa lishe hivy Wizara inaendelea kuyafanyia kazi na kutakuwa na mabadiliko kadili muda unavyozidi kusonga.
"Niwaahidi kwamba yote mnayopitia huko Wizara inayafahamu,inaendelea kuyafanyia kazi na tunaamini kwamba tutaona mambo mazuri kadili muda unavyokwenda".
Akisoma Risara yao Dkt Benson Sanga Mwenyekiti wa Maafisa lishe Nchini amesema kuwa pamoja na maboresho makubwa yanayo fanywa na Serikali kwenye Tasnia ya lishe lakini bado zipo changamoto chache zinazowakabili katika utendaji wao wa kazi ikiwemo suala la fedha za lishe kutoelekezwa katika afua za lishe na badala yake kupelekwa katika mambo mengine ambapo hupelekea kuathiri ufikiwaji wa jamii kwa wakati.
"Pajoma na kuwa na maboresho makubwa kwenye tasnia ya lishe lakini bado tunazo changamoto zinazotukabili katika utendaji wetu wa kazi ikiwemo muundo wa Utumishi wa kada ya Maadisa lishe nchini,kukosekana kwa maafisa lishe ngazi ya kata huvyo upo umuhimu wa Serikali kuajiri katika ngazi hizi ili kuongeza kasi ya utoaji wa huduma za lishe ikiwemo elimu na ushuri kuhusu lishe".
"Jambo lingine ni fedha za lishe kutoelekezwa katika afua za lishe,bado kumekuwa na fesha hii ya lishe katika Halmashauri kuelekezwa katika shughuli zingine zisizo za lishe hivyo hupelekea kuathiri ufikiwaji wa jamii kwa wakati ".
Bi Tedy Jumbe akitoa salamu za umoja wadau wa Maendeleo ambaye yeye ni Mwenyekiti mwenza amesema kuwa wataendelea kutafuta rasiliamali fedha na rasiliamali za kitaalam iki kuhakikisha jamii yetu ya Tanzania inakuwa na lishe bora.
"Tutaendelea kushirikiana katika kuvumbua,kuandaa,kuendeleza,kutekeleza na kufanya tathmini ya program za lishe,tunaendelea kuweka ahadi hiyo. Jambo la pili tutaendelea kutafuta rasiliamali za fedha na rasilimali za kitaalam ili kuhakikisha jamii uetu ya Tanzania inakuwa na lishe bora".
Katika kipindi cha miaka 23 Tanzania imepunguza udumavu kutoka asilimia 43.8 mwaka 1999, hadi kufikia asilimia 30 mwaka 2022 hii ni kupunguza kwa asilimia 13.8 katika kipindi hicho cha miaka 23 na asilimia 0.6 kwa mwaka.
Sasa lengo la Taifa ni kufikia asilimia 24 kwa mwaka 2025/2026.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...