-Ampongeza Askofu Pisa kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa TEC

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anasisitiza ufanyaji kazi kwa ushirikiano kati ya Serikali na Taasisi za Dini nchini ili kuendelea kujenga amani, umoja na mshikamano.

Amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi hizo ambao huleta matokeo chanya kwa ustawi wa Taifa.

“Tunashukuru tunapata ushauri, yapo mambo ambayo mnayafanya na kuiwezesha nchi hii iendelee, mshikamano wetu ndani ya nchi, umoja wetu ndio unaozaa utulivu na amani tuliyonayo”

Amesema hayo wakati akiwasilisha Salamu za Pongezi kutoka kwa Rais Dkt. Samia leo (Jumatano, Julai 03, 2024) kwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Wolfgang Pisa ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, kwenye makazi ya Askofu, Mtanda mkoani Lindi.

Amesema kuwa Serikali itaendelea kumpa ushirikiano wa dhati “wakati wote utakapokuwa na jambo ambalo unadhani Serikali inahitaji kushauriwa uwe huru na wakati wote unapoona kwamba unahitaji kuunganisha nguvu na Serikali, sisi tutakupa ushirikiano”

Ameongeza kuwa Serikali kwa upande wake imeshaagiza ushirikiano huo usiwe tu ngazi ya kitaifa bali uende hadi katika ngazi ya vitongoji “Tuendelee kuwa pamoja na kuja kwangu hapa nikuhakikishie tunaendelea kukupa ushirikiano”.

Kwa upande wake Askofu Pisa amemshukuru Rais Dkt. Samia Kwa salamu za pongezi za kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa TEC

Uchaguzi wa viongozi wapya wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) uliohusisha nafasi za Rais, Makamu wa Rais na Katibu ulifanyika tarehe Juni 21, mwaka huu, ambao waliochaguliwa ni Mhashamu Wolfgang Pisa Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi (Rais), Mhashamu Eusebius Nzigilwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Mpanda (Makamu wa Rais) na Padre Charles Kitima Padre wa Jimbo Katoliki la Singida (Katibu Mkuu).


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...