Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (​NBAA) imeendesha warsha kwa njia ya mtandao kwa Wakufunzi wa Vituo vya Kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi ili kuwaongezea ujuzi.

Akizungumza wakati wa kufungua warsha hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno amesema lengo la warsha hiyo ni kuwakumbusha majukumu yao ili kuendana na mitaala ya Bodi ambapo mwaka huu watahiniwa wanaanza kufanya mitihani ya Bodi hiyo kwa kutumia mitaala mipya.

Maneno amesema kwa Wakufunzi wa Vituo hivyo kwamba, kwa mwaka huu ambapo mitaala mipya imeanza kutumika wametakiwa kujadili vyema ili wanapokwenda kutoa elimu wawe na uelewa mzuri ili watahiniwa kufanya vyema kwenye masomo yao.
 
Pia amesema lengo kubwa la NBAA ni kuona wanapandisha kiwango cha ufaulu kwa mitihani mbalimbali pamoja na kuongeza kiwango cha uelewa ili kipindi wanapomaliza mitihani yao waweze kuwa wabobezi kwenye masuala ya Uhasibu na Ukaguzi.

Vilevile amewaasa wakufunzi wa vituo hivyo vya kufundishia masomo ya Bodi kuendesha masomo kwa njia ya mtandao ili kuweza kupunguza gharama za uendeshaji, kuwafikia wanafunzi wengi na kuendana na teknolojia.
Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Elimu na Mafunzo NBAA, Peter Lyimo akitoa mrejesho kuhusu namna mitihani ya Bodi ya mwezi Novemba itakavyofanywa baada ya  maboresho ya mitaala mipya wa masomo ya mitihani hiyo.
Mthibiti Ubora Mwandamizi kutoka NACTVET Bonaventure Ackles akitoa mada kwa wakufunzi wa vituo vya kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi  kuhusu namna nzuri ya kufundisha  watahiniwa kwenye masomo mbalimbali.
Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, CPA Dkt. Emmanuel Christopher akitoa elimu kuhusu njia bora ya kusimamia vituo vya kufundishia kwa Wakufunzi wa Vituo waliokuwa wanafuatilia kwa njia ya mtandao.
Mfanyakazi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), Sawa Ngendabanka akiwakaribisha wakufunzi wa vituo vya Kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi ambao walikuwa wakifuatilia Warsha hiyo kwa njia ya mtandao.
Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushauri Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC)  Dkt. Indiael Kaaya akitoa maelezo kuhusu namna ya kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufaulu watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi ili kuweza kuongeza ufanisi kwenye taaluma ya Uhasibu.
Mkufunzi CPA Rashid Mganwa akitoa maelezo kuhusu maboresho yaliyowekwa kwenye baadhi ya masomo kwa Wakufunzi wa vituo vya kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi waliokuwa wanafuatilia warsha kwa njia ya mtandao.
Mtaalamu wa Sarafu Mtandao, CPA Sandra Chogo akitoa elimu kuhusu sarafu mtandao kwa Wakufunzi wa vituo vya kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi waliokua wanafuatilia warsha kwa njia ya mtandao.
Afisa Idara ya Elimu na Mafunzo (NBAA), Salimu Kasumari akitolea ufafanuzi baadhi ya maswali yaliyokuwa yanaulizwa na Wakufunzi wa vituo vya kufundishia watahiniwa wanaotarajia kufanya mitihani ya Bodi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA), CPA Pius A. Maneno akizungumza kwa njia ya mtandao na wakufunzi wa vituo vya kufundishia watahiniwa wakati wa kufunga warsha hiyo.
Picha ya pamoja ya baadhi ya sekretarieti ya  warsha ya wakufunzi na wakufunzi wa watahiniwa wa mitihani ya Bodi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...