Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa Ziara ya Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi alipotembelea kituo cha Mkongo wa Baharini cha 2 Africa.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi  akimsikiliza Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano alipotembea mkongo wa Baharini uliopo Mbezi Beach Tangibovu jijini Dar es Salaam.

SERIKALI imesema Kipaumbele chake ni kuona idadi ya watumiaji wa data  inaongezeka katika jamii ya Watanzania.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati alipotembelea Airtel Tanzania na mkongo wa Baharini wa 2 Africa uliopo Mbezi Beach Tangibovu jijini Dar es Salaam leo Septemba 09, 2024. Amesema kuwa kwa sasa watu wachache wamefikiwa na matumizi ya data.

Amesema ili matumizi ya mkongo wa Baharini uwe mkubwa lazima simu janja ziwafikie watu wengi zaidi hadi vijijini.

"Watanzania wakishaweza kupata simu janja hizi kwa gharama nafuu basii matumizi ya mkongo huu wa baharini utakuwa ni makubwa zaidi." Amesema Mhandisi Maryprisca

Amesema manufaa zaidi yataonekana na vilevile kituo cha Airtel kitandelea kuwa Cha manufaa zaidi kwasababu watumiaji nao watakuwa wameongezeka kila iitwapo leo.

Pia imetoa wito kwa wadau mbalimbali ambao waweza kuingiza simu janja kwa gharama nafuu ili Kila mmoja aweza kupata  na kuongeza matumizi ya mkongo wa 2 Africa yaweze kuwa makubwa zaidi.

Amesema serikali inatoa ushirikiano mkubwa ambao unawezesha kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.

"Kama hapo zamani walikuwa wanatumia 2G kwamana watu walikuwa wanaweza kupata tu sauti kwahio Sasa wamekuja kuupgrade kwa 3G paka 5G kwalengo la kuboresha matumizi ya data Kama wananchi wanaweza kutumia intaneti kwa wingi lakini vilevile wanaweza kuboresha maisha na kuwa ya kidijitali zaidi." Ameeleza Mhandisi Maryprisca

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel, Beatrice Singano amefurahishwa na ziara ya naibu waziri Maryprisca Mahundi kutembelea Airtel Kama kampuni ya simu za mkononi.

"Ziara yake ilianzia hapa kwenye mkongo wa baharini wa 2 Africa Kama mnvyofahamu ni kwamba huu mkongo ambao ulizinduliwa na Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan mwaka jana mwezi wa nane sisi kwetu ni fahari kubwa Sana kwasababu mkongo huu unaunganisha mabara matatu nikimaanisha Afrika, Asia na Europe lakini vilevile una ukubwa wa km zaid ya 45 elfu." Ameleza

Amesema kuwa mkongo huu utaisaidia Tanzania kwa kuifungua na kumekuwa na mikakati mingi  pia  wanakukaribisha wawekezaje kuja nchini kwani miundombinu hiyo ni muhimu sana na inatoa mawasiliano lakini pia inaunganisha mabara mbalimbali.

Pia amewakaribisha wadau wote wa mawasiliano kwenda kununua 'capacity' uwezo kutoka kwenye kituo mkongo wa baharini wa 2 Africa kilichopo Mbezi Beach Tangibovu jijini Dar Es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...