Vijana Mkoani Kagera pasina kujali itikadi zao za Kidini wala Kisiasa wameusiwa kuchangamkia Fursa mbalimbali zinazojitokeza katika Mkoa wa Kagera ikiwemo Fursa za Kilimo, Ili kiondokana na wimbi la umaskini unaowasababisha Kuingia katika mihemko isiyokuwa ya lazima.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa Kagera Hajat Fatma Abubakari Mwassa akiwa Mgeni Rasmi wakati wa Uzinduzi wa Kikao cha Kikanuni cha Kawaida cha Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mkoani Kagera lilifanyika katika Ukumbi wa Sanad Hotel Wilayani Muleba Septemba 8 Mwaka huu.

Hajat Mwassa licha ya kuwahimiza Vijana hao kuacha Masuala yasiyokuwa ya tija kwao, amewakumbusha Vijana hao kuwa ni wakati Sasa wa kushirikiana kuinuana kifkira na Kiuchumi badala ya kutengenezeana ajali zisizokuwa na maana na huku akiwataka kuepuka matendo yasiyokuwa ya msingi kama vile michezo ya bahati nasibu, maandamano n.k

Aidha Mkuu wa Mkoa Hajat Fatma Mwassa ameongeza kuwa Mkoa Kagera kwa Sasa umekuja na mpango wa Mashamba Makubwa ya kilimo cha Kisasa cha Kahawa, hivyo kwa kuanzia Vijana watapatiwa Heka Hamsini, kwa ajili ya kilimo hicho ambapo Serikali itawezesha kila kitu kinachohitajika Vijana hao kulima, huku akiwasisitiza kuwa Tayari kujitokeza kuchangamkia Fursa hiyo ambapo kwa kuanzia mpango huo unaanza kutekelezwa Wilaya za Karagwe na Muleba.

Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Hajat Fatma Mwassa kupitia Baraza Hilo, amewakumbusha Vijana wa Mkoa Kagera kuwa Tayari kujitokeza kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Novemba Mwaka huu, Ili kugombea nafasi mbalimbali lakini pia kuwachagua Viongozi watakaofaa kuendelea mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...