Afisa mwamashishaji wa wanachama klabu ya Yanga Jimmy Kindoki (wa nne toka kushoto) akikabidhi cheti cha utambulisho wa tawi la Yanga USA ndani ya jengo la Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington, DC aliyekipokea cheti ni Afisa Ubalozi Malik Abdul(wa tatu toka kushoto) ambaye alishawahikua kiongozi wa Yanga huko nyuma. Baba Levo (kulia) na Saidi (wa kwanza kushoto) walikuwepo kushuhudia Makabidhiano hayo.
Tawi la Yanga USA linatoa shukrani za dhati kwa uongozi kwa kulitambua rasmi tawi hilo na kwa kipekee shukurani kwako Afisa Mwamashishaji Jimmy Kindoki kwa jitihada za makusudi ulizofanya kuhakikisha cheti hicho kinafika USA salama.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...